27 June 2012

Breaking Newzzzzz.........ANGALIA PICHA Dr.ULIMBOKA ALIVYO UMIZWA BAADA YA KUTEKWA



:Kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dkt. Steven Ulimboka Steven Ameokotwa Maeneo ya Mabwepande akiwa Amepigwa Mapanga na Hali Yake ikiwa ni Mbaya


 Juu ni taswira mbalimbali za Dr. Steven Ulimboka baada ya kuokotwa
Mkurugenzi wa Kituo cha haki za binadamu  Dk Hellen Kejo(kushot)akiwa na Dr. Steven Ulimboka muda mfupi baada ya kuokotwa akiwa amejeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana
Dr. Steven Ulimboka alipokua akieleza jambo kwenye mkutano wao(madaktari na Waziri Mkuu Mizengo Pinda Hivi Karibuni
....
UPDATE ya maelezo ya mkasa uliomkuta Dkt. Ulimboka:Dkt. Helen Kijo-Bisimba wa LHRC akinukuliwa katika EA Redio amekariri maelezo ya Dkt. Ulimboka ambayo pia yamesikika yakitamkwa na mwenyewe (Dkt. Ulimboka Steven), kupitia kituo cha redio cha CloudsFM, kwamba walikuja watu watatu waliovalia kiraia na kujitambulisha kuwa wao ni askari. Watu hao walimchukua na kumuingiza katika gari lisilokuwa na namba na kuanza kuelekea barabara ya Bagamoyo. Huko walimfunga kitambaa usoni, kamba mikononi na miguuni kisha wakampiga huku wakimwambia amekuwa akiwasumbua kwa muda mrefu na kama wangekuwa na sindano ya sumu wangemmaliza kabisa. ---
UPDATE:

Dkt. Ulimboka amefikishwa katika hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa huduma. Hali yake ni mbaya ila "stable".
------

Baadhi ya watu wa shirika la Tanzania Legal Human Rights Center (LHRC) walifanya juhudi za kumtafuta kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dkt. Ulimboka Steven aliyekamatawa (? tekwa) jana usiku.

Taarifa iliyotoka kwa mmoja wa wanaharakati hao inasema, walifanikiwa kumpata Dkt. Ulimboka kaitka eneo la Mwabepande, Dar es Salaam ) akiwa amefungwa kamba miguuni na mikononi, hajitambui (unconscious) na asiyeweza kuzungumza.

Taarifa hiyo inaongez akuwa, Dkt. Ulimboka alikuwa amepigwa vibaya sana katika sehemu mbalimbali za mwili wake na anahitaji matibabu ya haraka.

Juhudi zinafanywa kumpatia msaada unaohitajika Dkt. Ulimboka Steven.

6 comments:

  1. TANZANIA INAKOELEKEA SASA SIKO KABISA ,HAPA SERIKALI INAHUSIKA KWA ASILIMIA 100 KABISA,SASA TUSHAICHOKA HII SERIKALI DAWA NI 2015 KWENYE UCHAGUZI

    ReplyDelete
  2. mambo ya chama na uyo mtu wapi na wapi sababu wauguzi wanasababisha mamia ya kufa kwa ajili ya upumbavu mnaigomea serekari wakati taoumia masikini mnawagomea wakati familia zao mafua india kutibiwa

    ReplyDelete
  3. Navyofahamu mie tatizo halitatuliwi kwa vitisho, nadhani sasa ni muda mwafaka madakitari na wauguzi wote nchini kushikamana ili wawe kitu kimoja kudai haki zao.

    Inchi hii inautajiri wa kutosha ndiyo maana wakubwa kila siku wanakwenda Ulaya na Marekani, biashara ya kutwambia kuwa hakuna hela ya kuwaongezea wafanyakazi mishara ikome.

    Mungu ni mkubwa, wauwaji waliamini kuwa Dr. amekufa, kumbe sivyo, bahati nzuri tumesikia sauti ya Dr. na kuelewa kilichotokea, wale wenye akili wanajua kuwa ni mpango ulioratibiwa vyema, na ndiyo maana hata Hospitali ya Muhimbili ilivyoombwa kutoa gari kwenda kumchukuwa walikataa.

    Ni aibu kwa serikali na fedheha kubwa kuogopa kivuli chake, pia napenda kuiambia serikali yangu kuwa, sasa hivi watanzania wanaona na wanaielewa serikali yao jinsi inavyobahatisha mambo.

    ReplyDelete
  4. Je huo ni uungwana, ....nimwaza sana jambo hilo, lakini nikakumbuka usemi mmoja kuwa `yote uyaonayo, au kuyasikia sivyo yaweza yakawa sivyo yalivyo....vyovyote iwavyo, huo sio uungwana kabisa, tuongee tujadiliane, tutoe hoja, na sio kuumizana

    ReplyDelete
  5. TUSIWE WATU WA KUUNGANISHA MATUKIO NA KUTOA CONCLUSION PASPO SUBILA....SERIKALI ISILAUMIWE MOJA KWA MOJA KUWA UMEHUSIKA KWA PIA KUNA VISASI VYA SISI RAIA WENYEWE BAINA YA MTU NA MTU VINAWEZA TOKEA...DR. ULIMBOKA HAKUWA NA BODIGADI WA SERIKALI HADI TULAUMU KUWA NI SERIKALI.AKIPONA ATATOA MAELEZO VIZURI

    ReplyDelete
  6. Jamaani, tusilalamikie serekali huu kwasababu inawazekano kuwa wengine wamefanya hivyo ili serekali ionekane mbaya. Tu subiri kupata majibu za hakika. Mungu amsaidie daktari huyo na apone haraka

    ReplyDelete

Comments system

Disqus Shortname