14 February 2016

RAIS MAGUFULI AMFANYA KINGUNGE KUVUNJA AHADI YAKE...NAKUTOA KAULI HIIUtendaji wa Rais John Magufuli baada ya siku 100 tangu alipoanza rasmi kazi kama kiongozi wa ngazi ya juu zaidi nchini, umezua mijadala mingi huku asilimia kubwa wakimpongeza kwa kazi nzuri lakini wengine wamesimama na yao.
Muendelezo wa kuchukua maoni ya wanasiasa wakongwe, wadau wa maendeleo na wananchi wa kawaida umegonga mwamba kwa mwanasiasa mkongwe, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru na kupelekea kuivunja ahadi yake aliyoitoa awali kuwa angempima Rais Magufuli baada ya siku 100.
Kingunge ambaye alitangaza kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuiweka kando kadi yake namba 8 baada ya kukitumikia chama hicho kwa zaidi ya miaka 60, na kumpigia debe Edward Lowassa (Chadema), amekataa kuikamilisha ahadi yake ya kuuzungumzia utendaji wa Magufuli huku akieleza kuwa hakuna mtu wa kumlazimisha kuitimiza ahadi hiyo.
“Hata kama niliahidi kuzungumza baada ya siku 100 lakini hakuna mwenye uwezo wa kunilazimisha kuzungumza,” Kingunge anakaririwa na gazeti la Nipashe. “Sitazungumza, waulizeni wengine watasema lakini mimi naomba mniache,” aliseongeza.
Kingunge alitangaza kujeungua CCM kwa madai kuwa chama hicho kimevunja katiba wakati wa mchakato wa kumpata mgombea wake wa urais na kwamba imepoteza dira kwa kuacha misingi ya uasisi wake

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname