Wanawake wa jiji la Mwanza walionufaika na Mradi wa Manjano Dream Makers wakikisikiliza kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zinatolewa kwenye Mafunzo hayo Yanayoendelea Jijini mwanza..
Mafunzo ya kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano yameanza mkoani Mwanza. Washiriki wa fursa hiyo wanajulikana kama Manjano Dream Makers kwa lengo la kuwawezesha wanawake kiuchumi. Mafunzo hayo yamegawanyika katika awamu mbili. Awamu ya kwanza wanawake 30 wa Jiji la Mwanza Watapatiwa elimu kuhusu biashara, namna ya kukuza na kuendesha biashara na nidhamu ya kutunza pesa na mahesabu yaani 'financial literacy'.Pia washiriki watanufaika namna ya kutoa huduma nzuri na bora kwa wateja na jinsi ya kujiwekea akiba.
Mkufunzi wa Maswala ya Biashara Ndugu Felix Maganjila akiwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Shera Illusions Africa na Mkurugenzi wa Manjano Foundation Mama Shekha Nasser Wakati wa Mafunzo hayo leo.
Awamu ya pili washiriki watapatiwa elimu kuhusu matumizi sahihi ya Vipodozi hasa "Make-Up". Hapa washiriki watajua namna mbalimbali za kutumia vipodozi na namna ya kuwapamba maharusi na wakazi wa Mwanza na maeneo jirani kwa kutumia vipodozi.Mara baada ya mafunzo haya washiriki watapata fursa ya kukopeshwa mitaji kwa ajili ya biashara kwa lengo la kuwakwamua washiriki wote kuondokana na ukosefu wa ajira na kujikita katika kujiajiri. Mafunzo haya yanaratibiwa na Taasisi ya Manjano Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Shear illusions kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano. Mafuzo kama haya tayari yamesha wanufaisha wanawake 65 wa Jiji la Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja ya Washiriki wa Mafunzo ya Ujasiriamali kutoka Mkoa wa Mwanza.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo kutoka Mkoa wa Mwanza wameishukuru Taasisi ya Manjano Foundation kwa kuwapa nafasi hiyo na kuwaletea mrdai huu. Wakieleza zaidi wamesema walikuwa na hamasa sana tangu walipopata taarifa kwa wanawake wenzao wa mkoa wa Dar es salaam kunufaika na mradi huu na walikuwa wanasubiri kwa hamu kubwa sana mafunzo hayo.Wakiendelea zaidi wamesema wapo tayari kupigana na kujikita vizuri kupitia mradi huu kwa lengo la kujikwamua na kujiongezea kipato
No comments:
Post a Comment