Shirika la ndege Etihad limetunukiwa tuzo ya kifahari ya “Uvumbuzi katika Usafiri” katika hafla iliyoandaliwa na jarida la Travel Weekly ya kuwatunza wadau wa sekta ya usafiri dunia nzima huko Uingereza maarufu kama “Globe Travel Awards”. Hafla hiyo ilifanyika katikati ya wiki kwenye hoteli maarufu ya Grosvenor House, iliyopo Jijini London.
Kwa
kawaida tuzo hii hupewa kampuni ambayo imevumbua bidhaa au huduma yenye kuleta wimbi
la mabadiliko na maendeleo katika soko. Shirika la Etihad waliibuka washindi
baada ya jopo la wataalamu kuamua kwamba Shirika linastahili tuzo hii kutokana
na huduma yake ya “Makazi”- ambayo ni huduma binafsi ya kipekee duniani yenye
kutoa vyumba vitatu kwenye ndege ya Etihad. Huduma hii, iliyoleta mapinduzi
katika sekta ya usafiri wa anga,ni matokeo ya programu ya utafiti na maendeleo iliyoendeshwa
kwa miaka saba na kusimamiwa na timu nzima ya ubunifu kutoka kituo cha
Uvumbuzi, Jijini Abu Dhabi.
“Makazi”
yanayopatikana kwenye ndege za Etihad aina ya Airbus A380 yana ukubwa wa mita
za mraba 11 na ndani yake kuna sebule, bafu la pembeni, chumba kikubwa
cha kulala na mhudumu mmoja kwa kila chumba.
Shane
O’Hare, Makamu Rais wa Masoko wa Shirika la ndege la Etihad alisema: “Tunafurahishwa
na uamuzi wa jopo la wataalamu wa tuzo za Globe Travel, ambao ndio walipiga
kura ‘Makazi’ kuwa huduma bora iliyovumbuliwa katika sekta yetu. Vyumba hivi vimebadili
mitazamo ya wengi, vikiwapa fursa watu wa kawaida kufurahia huduma zinazopatikana
mara nyingi katika ndege binafsi tu.”
“Etihad
inathamini ushirikiano kati yake na soko la Uingereza, uhusiano ulioanza tulipozindua
safari zetu kuelekea na kutoka uwanja wa ndege wa Heathrow uliopo jijini London
mnamo mwaka 2004. Tumeinua hadhi ya usafiri ikiwa ni pamoja na kuzipa ndege zetu
muonekano halisia wa makazi ya kuishi na kuwapa wasafiri viwango vya hali ya
juu vya faragha na utulivu”.
Huduma
ya ‘Makazi’ inapatikana ndani ya ndege aina ya A380 zinazofanya safari zake
kati ya Abu Dhabi na London, New York pamoja na Sydney. SHirika la Etihad
linatazamia kuzindua huduma hii katika ndege ziendazo Mumbai na Melbourne mwaka
huu.
Etihad
ina timu maalumu ambayo kazi yake pekee ni kuhakikisha wanaochagua kusafiri na ndege
zao wanaweza kufuruahia vyumba ya ‘Makazi’ wapendavyo. Timu hii pia ipo karibu
na watoa huduma maalum waliopo kwenye vyumba hivi. Wateja wanapewa fursa ya
kufurahia huduma mbalimbali wakiwa wanasafiri na ndege hii ya Etihad zikiwemo;
kuweka oda ya mahala pa kula, burudani ndani ya ndege, matukio maalum kama
sherehe za kuzaliwa, maelezo kuhusu waendako na kadhalika. Watuapo, timu hiyo
maalum (VIP) huwasaidia wageni katika kufanya taratibu za kuwasili na usalama.
No comments:
Post a Comment