Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Barani Asia (AFC), na Makamu wa Rais wa FIFA, Sheikh Salman Bin
Ebrahim Al Khalifa leo ametembelea wizara ya Habari, Utamaduni na
Michezo, ambapo alifanya mazungmzo mafupi na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
Profesa Elisante Ole Gabriel.
Katika mazugmzo hayo, Sheikh
Salman ameielezea Serikali ya Tanzania nia ya FIFA kuendelea
kushirikiana na Serikali na TFF katika kuendeleza programu mbalibali za
maendeleo ya mpira hasa wa vijana na wanawake.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara,
Profesa Elisante ameihakikishia FIFA kuwa nia ya Serikali ni kuona
mpira unakua nchini na Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa TFF na
FIFA ili kufikia azama hiyo.
Aidha pia ametoa wito kwa AFC kusaidiana na TFF katika masuala ya exchange programmes ili vijana wetu wapate uzoefu wa nje.
Sheikh Salman na ujumbe wake
walitembelea ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) wakiwa
na Rais wa TFF, Jamal Malinzi, ambapo walikutana na Katibu Mkuu wa TFF,
Mwesigwa Selestine na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanya na
shirikisho, ikiwemo uwanja wa Karume, na Hostel zilizopo Karume.
Kiongozi huyo wa AFC, aliwasali
nchini jana mchana kwa matembezi ya siku mbili chini ya mwenyeji wake
Rais wa TFF, Jamal Malinzi na anatarajiwa kuondoka nchini kesho.
No comments:
Post a Comment