05 January 2016

NEWS ALERT:MWIGULU NCHEMBA ATIMUA VIGOGO WALIOKULA BILION 5.7 ZA UJENZI WA MACHINJIO YA KISASA RUVU


Wakati Taifa na Mataifa yakiendelea kutoa pongezi zao kwa serikali ya Rais.J.P.Magufuli kwa speed yake ya kuchapa kazi,Mawaziri wake pia wameendelea kuonesha namna walivyodhamiria kusimamia shughuli za maendeleo ya Nchi yetu.

Hii leo,Mh:Mwigulu Nchemba mwenye dhamana ya Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi amefanya ziara ya siku moja kwenye ranchi ya Taifa ya Ruvu kukagua ujenzi wa majengo ya machinjio ya kisasa ulioanza mwaka 2010.

Katika hali ya kusikitisha na kulazimu kuchukua hatua za kinidhamu,Mwigulu Nchemba amekutana na ubadhilifu wa Bilioni 5.7 ambazo zilitolewa kwaajili ya ujenzi wa jengo hilo,Fedha hizo zilizokuwa zimelengwa kuwezesha ujenzi wa machinjio hayo ya kisasa hazijafanya kazi kama ilivyokusidiwa.

Waziri huyo wa kilimo amekuta mradi huo umetelekezwa tangu mwaka 2010 bila kuendelezwa,Sababu za kutelekezwa kwa mradi huo zikidaiwa kuwa ni kutofautiana kwa mkandarasi na bodi ya NARCO(kampuni ya usimamizi wa ranchi za Taifa) hazikukubalika na Mh:Mwigulu Nchemba ambaye baada ya kusikiliza kwa makini ufafanuzi wa kutoka kwa viongozi wa ranchi hiyo aliamua ifuatavyo.

Kwanza,Mwigulu Nchemba amewatimua wakurugenzi wote wa bodi ya NARCO yenye dhamana ya kusimamia ranchi za Taifa kwa kushinda kukamilisha ujenzi wa mradi huo.Mbali na kushindwa,bodi hiyo imeutelekeza mradi huo na hivi sasa inapendekeza kujengwa kwa mradi mwingine kama huo ndani ya eneo hilohilo la ranchi ya ruvu.

Pili,Mwigulu Nchemba amesitisha utumishi wa Mkurugenzi mkuu wa ranchi za Tiafa kwa kushindwa kuchukua hatua za kusimamia ujenzi wa mradi huo hadi kukamilika kwake.

Pia,waziri huyo wa kilimo ameagiza kupitia vyombo vya sheria,wahusika wote walioshiriki ama kwa makusudi au kwa njia yoyote kuhujumu mradi huo usifanikiwe wanachukuliwa hatua haraka iwezekanavyo.

Mwisho,Nchemba amewaagiza wataalam wa wizara yake kuhakikisha ndani ya siku 7 wanampelekea ripoti ya thamani ya jengo lililokwisha kujengwa na fedha zinazotakiwa kumalizia ujenzi wa jengo hilo.

Sambamba na hatua hizo,Mwigulu ametoa rai kwa watumishi wote wa umma kuwa mstari wa mbele kusimamia kwa ufanisi na uzalendo miradi yote ya maendeleo ya nchi yetu,Mbali na hapo,serikali ya Magufuli haitakuwa tayari kuona mali ya umma inachezewa na kuibiwa wakati kuna watanzania wanaweza kusimamia mali hizo na kuziendeleza.
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi akiwasili kwenye mradi uliodumaa wa Ujenzi wa machinjio ya kisasa wa ranchi ya Ruvu mapema hii leo.

SOMA ZAIDI 

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname