Mume wa marehemu akiwa pembeni ya mwili wa mkewe.
Na Dustan Shekidele, UWAZI
MOROGORO: Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni! Kijana Said Ally Mwinyimvua anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro akidaiwa kumuua kwa kumcharanga mapanga mama yake mzazi, Sikuzani Said (70), kisa kikidaiwa kuwa ni kunyimwa wali (ubwabwa) na kupewa mdogo wake, Abass ambaye ni mziwanda, Uwazi linakupasha.

Tukio
hilo lililoacha majonzi, lilijiri wiki iliyopita nyumbani kwa familia
hiyo, Kijiji cha Kungwe, Kata ya Tomondo, Wilaya ya Morogoro Vijijini.
Uwazi
lilifika eneo la tukio na kuwakuta viongozi wa kijiji hicho kwa
kushirikiana na mgambo wakimpeleka mtuhumiwa huyo kwenye Kituo cha
Polisi Mkuyuni ambako anashikiliwa hadi sasa.
Abass anayedaiwa kumuua mamaake.
Kwa
upande wake, mume wa marehemu, Ally Mwinyimvua Dugulu ‘Mzee Kisauti’
(80), alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo alikuwa na haya ya kusema:
”Mimi
na mke wangu tumejaliwa kuzaa watoto tisa, wa kike wanne na wa kiume
watano. Wakike wote wameolewa huko mijini na wa kiume watatu wameoa pia
hukohuko mjini. Hapa nyumbani tumebaki na watoto wawili, Said na Abass
ambaye ndiye mtoto wa mwisho.
“Kwa
muda mrefu Said amekuwa akitulalamikia sisi wazazi kwamba tunampenda
zaidi mdogo wake kuliko yeye, jambo ambalo si la kweli.
“Hawa
watoto waliwekewa zamu ya kupika. Siku ya tukio ilikuwa zamu ya Said,
alipika ubwabwa, akaubeba wakaenda shamba. Ubwabwa mwingine waliubakisha
kwa ajili ya jioni. Mimi kutokana na kazi zangu nilibaki hapa nyumbani,
wakaniwekea ubwabwa wangu.
Polisi wakiwa eneo la tukio.
Saa 11 jioni, Abass na mama yake walirudi huku wakimuacha Said shambani.
“Saa moja usiku, Said alirudi, akaenda kwenye kabati na kukuta ubwabwa umekwisha. Alimuuliza mama yake, akamjibu kwamba mdogo wake amekula wote hivyo yeye ale kiporo cha jana, jambo ambalo lilimkera sana. Alichukua panga alilotoka nalo shamba na kuanza kumcharanga mama yake mwili mzima.

“Mimi
kutokana na uzee, nilishindwa kumsaidia mke wangu mpaka anakata roho
alikuwa akipiga kelele,” alisema Mzee Kisauti.Kwa upande wake, Abass
alipohojiwa, alisema alijaribu kumsaidia mama yake bila mafanikio kwani
kaka yake alitishia kumuua na yeye.
“lshu
kama ni ubwabwa angeniambia ningemuachia ale kuliko kumuua mama.
Nilijitahidi sana kumtetea mama lakini kaka alitaka kunikata na panga
hivyo nilikwenda kuita majirani ambapo walipofika tulikuta mama
ameshafariki dunia huku kaka akikimbia,” alisema Abass.
Alipoulizwa
kama kaka yake anakunywa pombe au kuvuta bangi, Abass alisema hatumii
vitu hivyo.Alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo, diwani wa kata hiyo,
Hamis lssa Msangale alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kusema:
“Mtuhumiwa
baada ya kumuua mama yake kwa kumcharanga mapanga zaidi ya 20 mwilini,
usiku huohuo alitoweka nyumbani na kwenda kujificha huku wananchi wenye
hasira wakimsaka kijiji kizima kwa lengo la kulipa kisasi.
“Kwa
bahati nzuri alfajiri, raia wema walitujulisha kwamba Said amepitiwa na
usingizi amelala chini ya mwembe. Nilimjulisha mwenyekiti wa kijiji,
tukachukua mgambo tukaenda kumkamata na kupita naye vichakani mpaka
Kituo cha Polisi Mkuyuni tukiwakwepa wananchi wenye hasira,” alisema
kiongozi huyo.
Akaendelea:
“Kwa sasa tukio hili ndiyo gumzo kata nzima na ni tukio la kwanza
kutokea kwenye kata yetu. Tunashukuru mtuhumiwa tumemkamata na muda huu
tunafanya utaratibu wa kumzika marehemu kwenye makaburi ya kitongojini
hapa.”
No comments:
Post a Comment