Hukumu
ya Kesi iliyofunguliwa na wapambe (wapiga kura) wa mzee Wasira ya
kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la Bunda yaliyompa ushindi Mhe Ester
Bulaya imekamilika.
Katika hukumu hiyo Mhe Ester Bulaya kaibuka kidedea baada ya pingamizi lake aliloliweka Katika kesi hiyo kukubaliwa na mahakama hiyo na hivyo kufanya kesi hiyo kutupiliwa mbali.
Katika hukumu hiyo Mhe Ester Bulaya kaibuka kidedea baada ya pingamizi lake aliloliweka Katika kesi hiyo kukubaliwa na mahakama hiyo na hivyo kufanya kesi hiyo kutupiliwa mbali.
Mbunge wa Bunda amejihakikishia
kuwatumikia wananchi wake bila Muwashawasha, baada ya kesi
Iliyofunguliwa na Masato Wassira Kutupiliwa mbali na mahakama.
Hiki ndicho alichokiandika Mh. Mbunge Ester Bulaya;
''Nimemshinda Wasira kwa wananchi na leo nimemshinda mahakamani. Mahakama imetupilia mbali kesi yake dhidi ya Ushindi wangu.'
Wassira alipinga matokeo ya Uchaguzi
jimbo la Bunda Mjini Mahakamani kuwa matokeo hayo sio halali na kwamba
kuna hujuma zimefanywa ili kumuangusha na kumpendelea Esther Bulaya.
Wassira ambaye pia alikuwa Waziri wa
Chakula na Ushirika, alidai kuwa matokeo yaliyotangazwa yana kasoro
kubwa ikiwa ni pamoja na idadi ya kura zinazoonekana kuwa zilipigwa
zinazidi jumla iliyopo kwenye matokeo hayo.
Alisema kuwa msimamizi wa uchaguzi
alimhujumu kwa kuongeza tarakimu kwenye matokeo hayo na kwamba tarakimu
hizo zilipelekea idadi ya wapiga kura kwenye kituo kimoja kuzidi idadi
iliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Mwanasiasa huyo mkongwe pia
alidai kuwa msimamizi wa uchaguzi alitangaza matokeo bila kuzingatia
sheria ya uchaguzi.
Wakili upande wa mjibu maombi Tundu Lisu (mwenye miwani) akizungumza, Kushoto ni mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini Esther Bulaya.
Walioleta maombi (Mlalamikaji) katika
kesi hiyo wametajwa kuwa ni wapiga kura wa jimbo hilo la Bunda Mjini
ambao walikuwa wakiiomba Mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi huo
katika jimbo hilo kutokana na uchaguzi huo kukumbwa na kasoro mbalimbali
ikiwemo uchaguzi kutokuwa huru pamoja na idadi ya wapiga kura
kutofautiana na idadi ya waliojiandikisha katika daftari la kudumu la
wapiga kura.
Madai hayo yalipingwa na upande wa
Mjibu Maombi (Walalamikiwa ambao ni Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini
pamoja na Mwanasheria wa Serikali) uliokuwa ukiongozwa na Wakili Tundu
Lisu. Upande wa Mleta maombi ulikuwa ukiongozwa na Wakili Constantine
Mutalemwa
No comments:
Post a Comment