Kitendo cha ndege ndogo (3) za serikali kuuzwa kwa Shilingi laki tano (TZS 500,000/-) kila moja chawakera wananchi, Waziri naye ashangaa!
Kitendo
cha ndege ndogo (3) za serikali kuuzwa kwa Shilingi laki tano (TZS
500,000/-) kila moja chawakera wananchi, Waziri naye ashangaa!
- Ndege hizo kuwa ni 5H-MRN, Cessna 185 nyingine ni 5H-MRF, Cessna 185 na nyingine aina ya 5H-MRP piper Super Cub
- Waziri Chiza aja juu na kuhoji iweje ndege hizo ziuzwe kwa Sh 500,000 kila moja
WAZIRI
wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi Christopher Chiza jana
alishikwa na butwaa, pale alipopewa taarifa ya kuuzwa ndege tatu za
Serikali, ambazo zilikuwa katika Kituo cha Kilimo Anga kwa kiasi cha
Sh500,000 kwa kila moja.
Ndege hizo, tatu zilikuwa zikitumika katika udhibiti wa wadudu waharibifu wa mazao.
Akisoma
taarifa ya kituo hicho mbele ya Waziri Chiza, Mhandisi Mkuu wa Ndege
wa kituo hicho,Gideon Mugusi,alizitaja ndege hizo kuwa ni 5H-MRN,
Cessna 185 nyingine ni 5H-MRF, Cessna 185 na nyingine aina ya 5H-MRP
piper Super Cub ambazo zilianguka katika vipindi tofauti.
“Ndege
zote tatu ziliharibika lakini Shirika la Bima la Taifa(NIC), walilipa
Serikali kupitia katibu mkuu wa Wizara ya Kilimo, kulingana na viwango
vya bima vilivyokuwa vikilipwa na wizara”alisema Mugusi.
Hata
hivyo alisema tangu kuanguka na kuuzwa kwa ndege hizo,shughuli za
kituo hicho, Kimekuwa zikidorora kwani marobani karibu wote wameondoka
na kituo kimebaki na ndege moja tu ambayo pia ni mbovu na kibali cha
kuruka angani kimekwisha.
Alisema kwa sasa kutokana na kukosekana kwa ndege, gharama za uendeshaji
wa shughuli za kituo zimekuwa ni kubwa mno kwani wanalazimika
kukodisha helikopta na gharama zake zimekuwa zikipanda mwaka hadi
mwaka.
Waziri aja juu:
Kutokana na maelezo hayo, waziri Chiza alikuja juu na kuhoji iweje ndege hizo, ziuzwe kwa Sh 500,000 kila moja.
Waziri huyo, pia alihoji iwapo ndege hizo, zilifutwa kwenye orodha ya
kumbukumbu za Serikali kama hazifai kwa matumizi pia kama ufutwaji wake
ulifuata sheria na kanuni za Serikali.
“Leo
sikuja kukamata mchawi, ila mimi binafsi nitafuatilia ili kuona kama
sheria zilifuatwa au kama ndege zimeuzwa bila kufuata sheria” alisema
Chiza.
Awali alisema Serikali ina mpango wa kufufua kitengo hicho na kwa kuanzia tayari imetoa fedha za kununua ndege moja.
“Naagiza
mfanye mchakato haraka wa kununua ndege hii, hatutaki tena ukiritimba
kwani nia ya Serikali ni kufufua kituo hiki,”alisema Chiza.
Alisemakituo hicho ndiyo pekee katika nchi za Afrika ya Mashariki
chenye uwezo wa kutoa huduma hiyo ya kilimo anga na kama ndege zikianza
kufanya kazi, basi zitaweza kukodiwa na nchi jirani.
Kituo
cha Kilimo Anga kilianzishwa na wizara ya kilimo ,ikishirikiana na
Umoja wa Mataifa kupitia Shirika la UNDP na FAO mnamo mwaka 1979 na
lengo kubwa lilikuwa ni kuimarisha utoaji huduma katika sekta ya kilimo
katika kupambana na visumbufu vya mimea wahamao(migratory pest control)
source jamiiforums