29 January 2016
Bweni la Shule ya Sekondary Edward Lowassa Lateketea kwa moto
Bweni la Wavulana katika shule ya Sekondari Edward Lowassa iliyopo katika wilaya ya Monduli mkoani Arusha limetetekea kwa moto usiku wa kuamkia alhamisi ya wiki hii na kusababisha hasara ya vitu mbalimbali ikiwemo mali za wanafunzi na majengo vyenye thamani zaidi ya shilingi milioni 200
Moto huo ambao chanzo chake kinasadikiwa ni wanafunzi kukata nyanya za umeme juu ya dari kwa lengo la kucharge imeelezwa kutosababisha madhara yoyote kwa wanafunzi.
Bweni hilo ambalo limeanza kuungua kwa moto majira ya saa moja na nusu za jioni wakati wanafunzi wakiwa katika masomo ya jioni hakuna madhara yotote kwa mwanafunzi ambayo yameweza kuripotiwa
Mkuu wa Wilaya ya Momduli Fransisi Miti akizungumza wakati alipotembelea eneo hilo amewataka wazazi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki huku akilazimika kuifunga shule hiyo kwa siku saba wakati wanatafuta wadau watakaoweza kujenga bweni hilo
Awali Mkuu Mkuu wa Shule hiyo amewaomba wadau mbalimbali wa Elimu kujitokeza kusaidia ujenzi wa bweni ili wanafunzi waweze kurudi shuleni mapema na kuendelea na masomo
Majanga ya moto kwa shule za Sekondari kwa Wilaya ya Monduli yemeendelea kujitokeza mara kwa mara ambapo hii ni shule ya nne sasa kwa kipindi cha miaka 2
Labels:
lowassa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment