ITV imeshuhudia mamia ya watu wakiwa wamefurika katika mashine ya
kusaga nafaka inayomilikiwa na Bi.Jamira Abdu Mkazi wa chato ambaye
amemtaja marehemu kuwa anafahamika kwa jina la Juma Saidi alikuwa
akifanya kazi ya kusaga nafaka katika mashine hiyo zaidi ya miaka saba
na kusema kwamba hivi karibuni marehemu alikuwa na ugomvi na mkewake
ambapo alihama nyumbani kwake na kuanza kulala mashineni hapo.
Baadhi ya wananchi wanaomfahamu marehemu Juma wamesikitishwa na
tukio la mauaji ya kinyama na kuiomba serikali kuimalisha ulinzi na
wengine wakuiomba kurejeshwa kwa jeshi la jadi Sungusungu kwa lengo la
kukomesha matukio ya kihalifu.
Alipotakiwa kuthibitisha tukio hilo mwenyekiti wa kamati ya ulinzi
na usalama ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Chato Bw. Shabani Ntalambe
hakuwa tayali kuzungumzia suala hilo kwa madai kuwa anasimamia usafi wa
mazingira ambapo ITV imelazimika kuzungumza na afisa mtendaji wa kijiji
cha Muungano na diwani wa kata ya Muungano ambao wamethibitisha kutokea
kwa mauaji ya kinyama.
No comments:
Post a Comment