Naamini viongozi wa CHADEMA wanafika hapa JF, lkn pia najua wanachama
ana wafuasi wapo wengi hapa JF. Kwa muda mrefu CDM imetusaidia
watanzania kutufumbua macho wakati ufisadi ukitamalaki. Yaliyopita si
ndwele tigange yajayo.
Tangu uchaguzi umalizike CDM imekuwa ni chama cha matukio, kwa kizungu
reactive to the incident. Tumeona CDM ilivyotumia msiba wa MAWAZO (MUNGU
AMREHEMU) kwa sababu kama amekufa kwa sababu ya tofauti za kisiasa
watanzania tunaelekea kubaya. Lakini CHADEMA kilitumia msiba huu
kujipatia umaarufu km kwamba CHAMA CHA MAPINDUZI ndicho kiliwatuma
waharifu kumuua kamanda MAWAZO, sitaki kuamini km CCM kama chama wana
uwezo wa kufanya haya kwaani uchaguzi umeisha na walishinda kwa 95%
kanda ya ziwa.
Kabla ya hili la mawazo CHADEMA walikuwa wanatafuta sympathy ya wananchi
kwa kutumia kesi mbalimbali mfano ni kesi ya SHEKH PONDA aliyeshinda
kesi hapo jana. Kuna wakati Fulani alikuwa akitetewa na wakiri maarufu
wa CHADEMA pale Morogoro. Sijui kwa nini CDM waliingiliaje kesi hii
kidogo wamuharibie mshitakiwa kwaani serikali ingeona kama vile alikuwa
anatumiwa na CHAMA.
Jana baada ya kupata ushindi dhidi ya serikali niliona viongozi wote wa
CDM wakiongozwa na aliyekuwa mgombea ubunge ndugu MARCUS ALBAN
waliongoza waaumini kutoka eno la mahakama mpaka eneo la msikiti wa
MUNGU MMOJA.
Wakati wa kampeni tuliskia aliyekuwa mgombea Urais kupitia CHADEMA
Mheshimiwa Edward Lowassa kuwa kama angechukua dora basi angewaachia
huru watuhumiwa mbalimbali wakiwamo Shekh Farid na Babu seya. Kwa kifupi
kama hawana makosa wanastahili kuachiwa kwa mujibu wa sheria lakini
siyo kwa mujibu wa matakwa ya mtu.
USHAURI KWA CDM NA UPINZANI:
Fanyeni vitu endelevu na vinavyoenekana, yaani sustainable and tangible
la sivyo mtasahaulika, kumbukeni watanzania ni wepesi sana wa kusahau,
jumrisha na kasi ya serikali ya awamu ya tano ambayo imezichukua sera za
upinzania kuzifanyia kazi hasa ile ya ufisadi iliyotupwa baada ya
kumpkea LOWASSA kitendo kilichoitwa na kubadili gear angani.
ACHENI KUTUMIA MATATIZO KATIKA JAMII KUTAFUTA UMAARUFU WA KISIASA.
No comments:
Post a Comment