28 December 2015

BREAKING NEWZZZ.....MWANAMUZIKI CHIPUKIZI AUWAWA KWA KUPIGWA RISASI NA ASKARI


Umilikaji wa silaha kwa vijana wadogo umeongezeka siku za hivi karibuni, kiasi cha kusababisha vifo kwa vijana wengi wenye vipaji wanaochipukia.
Katika tukio lililotokea huko North Carolina Marekani,  rapper chipukizi aliyeanza kufanya ‘poa’ kwenye ‘game’ Donkey Cartel alipigwa risasi na polisi mpaka kupelekea umauti kumkuta.
Rapper huyo ambaye jina lake halisi ni Daquan Antonio Westbrook, alipigwa risasi mfululizo kwenye ‘Mall’ moja mjini humo baada ya kumuelekezea mtutu wa bunduki askari mmoja aliyekuwa lindoni.
Ilikuwa ni baada ya ugomvi wa vijana watano, ndipo ikamfanya rapa huyo atoe silaha yake.
Alikuwa akitamba mjini humo na mixtape zake mbili, ikiwemo moja maarufu aliyoiita Convicted Felon With a Weapon

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname