16 November 2015

WAZIRI MKUU HACHAGULIWI KWA KURA ZA MAONI WALA KWA MITANDAO YA KIJAMII - MWAKYEMBE


Na Lilian Lundo
MAELEZO
DODOMA
15.11.2015
 
Mbunge Mteule wa Jimbo la Kyela,  Dkt. Harrison Mwakyembe amesema Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania  atatokana  na uteuzi utakaoidhinishwa na  Bunge na si taarifa zilizopo sasa katika mitandao ya kijamii.
 
Dkt. Mwakyembe ambaye amewahi kuwa Waziri wa Uchukuzi katika Serikali ya Awamu ya Nne, alisema kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi,  Waziri Mkuu anateuliwa na Rais ambaye huwasilisha jina hilo kwa Spika wa Bunge na baadaye kupigiwa kura na Wabunge.
 

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname