14 November 2015

TAIFA STAR WATOKA SARE NA ALGERIA

Hatimaye mchezo wa kwanza wa kuwania kufuzu fainali za michuano ya Kombe la Dunia2018 zitakazofanyika Urusi kati ya timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars dhidi ya timu ya taifa ya Algeria Mbweha wa Jangwani ndio umechezwa leo November 14 uwanja waTaifa Dar Es Salaam, mchezo wa marudiano utachezwa November 17 Algiers.
DSC_0111
Mbwana Samatta akijaribu kumtoka Mandi Issa wa Algeria
Takwimu za mchezo huo zilikuwa rafiki kwa upande wa timu zote mbili kwani kabla ya kupigwa mchezo huo, kwa takwimu za hivi karibuni Taifa Stars iliwahi kucheza naAlgeria September 3 2010 Algiers na kutoka 0-0 katika mchezo wa AFCON, lakini September 3 2011 Dar Es Salaam Stars ilitoka sare ya goli 1-1 kitu ambacho kilifanya timu zote kuwa na rekodi ambazo haziwezi kumtisha mwenzake.
DSC_0120
Farid Mussa akipiga mpira ambao ulizuiliwa kwa mkono na Mandi Issa ila haikuwa penati
Licha ya kuwa Taifa Satrs ilikuwa katika nafasi za chini katika viwango vya FIFAukilinganisha na Algeria, hiyo haikuifanya Taifa Stars ishindwe kucheza soka safi, kipindi cha kwanza Stars ilianza kwa kukosa magoli kabla ya dakika 43 Elias Maguli kupachiga goli la kwanza ambalo lilidumu kwa dakikza zote 45.
DSC_0083
Mashabiki hawakuacha kuwapongeza wachezaji wa TP Mazembe Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu kwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kipindi cha pili Taifa Stars walirudi kwa kasi na Mbwana Samatta akadhihirisha ubora wake wa kupachika magoli baada ya dakika 54 kupachika goli la pili kwa Stars, furaha ya watanzania ilianza kupotea dakika ya 71 Sliman Islam alipachika goli la kwanza la Algeria na dakika mbili mbele akapachika goli la pili, hadi dakika 90 zinamalizika Taifa Stars 2-2 Algeria.
DSC_0106
Wachezaji wa Taifa Stars wakifurahia goli la Mbwana Samatta
DSC_0064
Thomas Ulimwengu katika harakati za kumpita Ghoulam Faouzi wa Algeria
DSC_0075
Elias Maguli na Nadir Haroub wakifurahia goli la kwanza la Taifa Stars
DSC_0085
Mashabiki wa Tanzania wakati wa mapumziko walivyokuwa wanafurahia goli la Maguli
DSC_0058
Thomas Ulimwengu akijaribu kumtoka Mandi Issa wa Algeria
DSC_0052
Kocha wa makipa Peter Manyika Senior akisali na golikipa wa Taifa Stars Ally Mustapha kabla ya mchezo kuanza

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname