TUJIUNGE NA CHANZO JIJINI NAIROBI
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini kilichoambatana na mwigizaji huyo jijini Nairobi, Kenya katika matibabu, staa huyo alifikia hatua ya kwenda hospitali baada ya kuzidiwa na maumivu makali yaliyosababishwa na uvimbe kwenye mguu wake.
GHARAMA MIL. 8
Kikizungumza na Ijumaa Wikienda baada ya kuwasili katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya, Alhamisi iliyopita, Wastara alipokelewa na madaktari wa hospitali hiyo na kuanza kumpatia huduma ndogondogo.
Kilisema kuwa mapema Siku ya Ijumaa, Wastara alifanyiwa upasuaji pamoja na matibabu yaliyodumu kwa saa kadhaa yaliyogharimu shilingi milioni 8 za Kibongo.
MAUMIVU MAKALI
“Kiukweli mwenyewe (Wastara) amesema maumivu aliyoyapata ni makubwa na makali mno.
“Mtu ulikuwa ukimuangalia unahisi kabisa uchungu anaoupata kama unaupata wewe. Usiku hakuweza kulala zaidi ya kugugumia kwa maumivu makali. Dah! Wastara ni mwanamke anayepitia mitihani mizito sana katika maisha yake,” kilisema chanzo hicho.
HUYU HAPA WASTARA
Baada ya kupata taarifa hizo, gazeti hili liliwasiliana na Wastara kwa njia ya simu ambapo alisema anamshukuru Mungu kwa kuwa zoezi limefanikiwa ingawa anahisi maumivu makali ila anaamini Mungu atampitisha salama.
“Mungu ni mwema na ninamshukuru naendelea vizuri kidogo na zoezi limefanikiwa ila bado nina maumivu sana ambayo nimeyapitia kwa saa karibia ishirini na nne, naamini nitakuwa vizuri baada ya muda mfupi,” alisema Wastara kwa sauti ya chini huku akiwashukuru wote wanaomuombea apone haraka.
TATIZO LILIANZIA KWENYE KAMPENI
Tatizo la Wastara la kukatwa mguu kwa mara ya pili lilikuja hivi karibuni alipokuwa kwenye Kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) zilizofikia tamati Oktoba 24, mwaka huu.
WASTARA AMEFIKAJE HAPA?
Machi 12, 2009, wakati huo wakiwa wachumba, Wastara na marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ walipata ajali ya pikipiki maeneo ya Tabata, Dar ambapo mwanamama huyo alivunjika mguu wa kushoto.
Baadaye mguu huo ulikatwa baada ya kuharibika ambapo aliwekewa wa bandia ambao nao umekuwa ukimsumbua hadi alipoamua kwenda kuuondoa na kuwekewa mwingine.
Chanzo: GPL
No comments:
Post a Comment