16 November 2015

MAKAMU WA RAIS AWAPA MOYO WACHEZAJI WA TAIFA STARS KUELEKEA MCHEZO WA MARUDIANO


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kumpongeza Nahodha wa Timu ya Taifa Stars, Nadir Haroub 'Canavaro', baada ya mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya makundi Kombe la dunia kati ya Taifa Stars na Algeria  uliochezwa jana. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 2-2, mabao ya Stars yalifungwa na Elias Maguli na Mbwana Samatta. 
Akizungumza na wachezaji hao baada ya mchezo huo, Mhe. Samia,aliwataka wachezaji na viongozi wa Stars kutovunjika moyo kutokana na matokeo ya mchezo huo, na kuwataka kuongeza juhudi na kujituma zaidi katika mchezo wa marudiano ili ukweza kupata matokeo mazuri zaidi.
''Japo mmefungwa lakini tumewaona jinsi mlivyojituma, msivunjike moyo na matokeo ya mchezo, kwani tumeowana mlivyocheza kwa kujituma, hivyo naamini hata ugenini mtaweza kupata matokeo mazuri zaidi mkiwa na moyo huo huo wa utaifa, juhudi na kujituma,
Mtangulizeni mungu kwa kila jambo na kwa uwezo wake naamini mtaenda kufanya vizuri katika mchezo wa marudiano, na nawatakieni safari njema leo usiku kuelekea mchezo huo wa marudiano, sisi wazee wenu na Watanzania wote tupo nyuma yenu tunawaombe muweze kuwatoa waarabu hawa wenye fitina kali katika mchezo wa Soka''. alisema Mhe. Samia 

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname