Rais Dk John Pombe Magufuli.
WAKATI Rais
John Pombe Magufuli akitegemewa kutangaza Baraza la Mawaziri wakati
wowote kuanzia sasa, matumbo ya wabunge yamepata moto wakijiuliza kama
watawezana na kasi yake endapo watateuliwa kuwemo.
Magufuli, ambaye Rais
Mstaafu Jakaya Kikwete alimuita Tingatinga, ameweka wazi katika hotuba
yake kwa Bunge kuwa hatamvumilia mtu mzembe na mvivu na kwamba
watakaobainika kujihusisha na rushwa au ufisadi, watashughulikiwa.
Ingawa wabunge karibu wote
walikuwa wakimshangilia kwa nguvu wakati wa hotuba yake hiyo, inadaiwa
hamu ya kupata ulaji wa uwaziri inawafanya baadhi yao kuingiwa na woga,
kwani ufanyaji kazi wa mazoea ndiyo unaowatesa.
“Nakuambia hapa wabunge,
hasa wale wenye ndoto za kuteuliwa uwaziri wana wasiwasi kama wataweza
kweli kwenda na kasi ya huyu jamaa, maana anaonekana kuwa siriaz sana na
kazi. Hili liko wazi maana wengi walizoea kuona nafasi za juu kiuongozi
wanazitumia kwa masilahi yao,” kilisema chanzo chetu katika viwanja vya
Bunge mjini Dodoma.
Inadaiwa wengi wa
wanaotegemea kupata uwaziri wana hofu kwa sababu wanaamini mzigo
watakaopewa utakuwa mkubwa kuliko tabia na hulka zao.
Rais Magufuli ameahidi
kuteua Baraza dogo la Mawaziri litakalokuwa limesheheni wachapakazi na
katika kukabiliana na vitendo vya rushwa na ufisadi, alisema kazi hiyo
ataifanya kwa dhati.
Hata hivyo, mbali na jina
la Tingatinga hivi sasa mtaani amepewa jina jipya la Mtumbua majipu
licha ya kuwa kitendo hicho huleta maumivu.
No comments:
Post a Comment