08 October 2015

SHINDANO LA SERENGETI MASTA LAHITIMISHWA KANDA YA ZIWA

Wadau wa bia ya Serengeti Premium lager wakigonga cheers, ndani ya baa ya Shooters iliyopo barabara ya Airport jijini Mwanza wakati wa shindano la mwisho la kumtafuta Serengeti Masta wa jumla kwa mikoa ya kanda ya ziwa katika baa hiyo. Kampeni ya “Serengeti Masta” imedumu katika kanda hiyo kwa takriban miezi miwili na imezunguka baa kwa baa kusaka washindi mbalimbali wanaotambua ladha halisi ya bia hiyo lakini pia imetoa elimu kwa wateja wake kuhusiana na chapa hiyo namba moja kutoka SBL.

Mshindi wa jumla washindanola Serengeti Masta kwa wakazi wa kanda ya ziwa Said Kanolo (kushoto) akipokea fedha taslim Tsh. 100,000/= kutoka kwa Afisa mauzo wa Kampuni ya bia ya Serengeti Joan Semguruma, (kulia) wakati wa shindano la mwisho kwa kanda ya ziwa la bia hiyo lililofanyika katika baa ya Shooters iliyopo Barabara ya Airport jijini Mwanza. Ushindi wa jumla wa Bw. Kanolo kwa wateja wa kanda ya ziwa umekuja baada ya kuwashinda wateja wengi walioshiriki katika kutambua ladha halisi ya bia hiyo na kuielezea kwa undani ambapo mwanzo wa Kampeni alishinda Tsh. 50,000/= pamoja na zawadi nyingine kutoka bia ya Serengeti Premium Lager katika baa ya Cross parkjijini Mwanza nakufanikiwakutingafainali. Kampeni hii imezunguka katika baa mbalimbali za kanda ya ziwa ikiwaburudisha wateja wa bia hiyo na kuwafundisha wahudumu wa baa mbalimbali juu ya utoaji huduma kwa wateja.

Mshindi wa jumla wa shindano la Serengeti Masta Said Kanolo (katikati) akifurahi na wadau wa bia ya Serengeti Premium Lager, wakati wa shindano la mwisho la Serengeti Masta kwa wateja wa kanda ya ziwa lililofanyika katika baa ya Shooters iliyopo barabara ya Airport jijini Mwanza. Kampeni hiyo ya Serengeti Masta imedumu katika kanda hiyo kwa takriban muda wa miezi (2) sasa ikiwakutanisha wateja na meneja wa bia hiyo katika kujifunza kwa undani kuhusiana na bia hiyo ambapo zawadi mbalimabli zilipatikana

Mshindi wa mwisho wa shindano la Serengeti Masta kwa wakazi wa kanda ya ziwa Said Kanolo, akionyesha pesa zake alizokabidhiwa, kwenye shindano la mwisho la kumtafuta Serengeti Masta wa mwisho wa kanda hiyo ambalo lililofanyika katika baa ya Shooters iliyopo barabara ya Airport jijini Mwanza. Shindano hilo limemalizika rasmi kwa wakazi wa kanda ya ziwa likiwa limetembelea baa mbalimbali katika kanda hiyo na kuwafikia wateja wengi zaidi walioweza kuitambua ladha ya bia ya Serengeti Premium Lager na kutuzwa zawadi mbalimbali pamoja na fedha taslim.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname