03 October 2015

PICHA ZA AJALI YA GARI LA MGOMBEA UBUNGE CHADEMA

GARI YA MGOMBEA UBUNGE WA CHADEMA JIMBO LA NYASA LAPINDUKA
Kamanda Ngwata kapata ajali mbaya baada ya dereva wake kuingia porini na kusababisha kifo cha Kamanda Pompi kutoka Mbozi Mbeya ambaye alikuwa huko kikazi. 
Kamanda Ngwata na dereva wake wamejeruhiwa na wako hospitali ya Wilaya ya Nyasa kwa matibabu lakini taarifa nilizopata sasa Mgombea wako njiani kumuamishia Litembo Hospital hali yake ni mbaya na amekata kauli.
Ilikuwa ni usiku walikuwa wanaelekea kijijini kwa ajili ya kampeni za leo na inasemekana kuwa watu watatu wenye silaha walitaka kuwateka njiani katika kukabiliana na hilo ndio Dereva akayumba na gari likaingia korongoni..

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname