Hii imetokea jioni ya leo katika viwanja vya Mnazi mmoja,Zanzibar katika safari yake ya kuwaomba Watanzania wamchague kuwa Rais wa Tanzania.
Magufuli amewakikishia wananchi wa Zanzibar atahakikisha anaulinda Muungano bila kutetereka.
Magufuli amesema yeye ni mpole sana lakini hana mchezo katika kusimamia sheria na taratibu za nchi.
''Mimi siyo mwanasiasa mzuri sana lakini vilevile sipendi mwananchi yoyote kuonewa au kupuuzwa''. alisema.
Dk. Magufuli amemalizia kwa kusema ‘’Natoa pole kwa Mh.Jerry Silaa kwa kuondokewa na baba yake mzazi Capt.William Silaa. Mungu awape familia moyo wa subira na uvumilivu’’
‘’Mungu pia awape ndugu, marafiki na jamaa moyo wenye subira na heri kwa kuondokewa na Deo Filikujombe
No comments:
Post a Comment