21 October 2015

MASHALI AMDUNDA BIGRIGHT NA KUMPORA SIMU NA PESA


Bondia Thomas mashale wa manzese jijini Dar es salaam alifanya kitendo cha kusikitisha na kushangaza umma katika ukumbi wa friends corner uliopo Manzese ,pale alipomvamia katibu wa ngumi za kulipwa nchini Ibrahim Kamwe (bigright) kumpiga na kumpora simu na pesa. Akizungumza na vyanzo habari hizi Ibrahim kamwe alisema.”Nilikuwepo ukumbini  hapo friends corner nikishuhudia mpambano wa Jonas Segu na idd Pearali kwa kuwa watu walikuwepo ni wengi mno na pale mbele kulikuwa na fujo za ushangiliaji  nikaona ni bora nirudi nyuma kabisa ili nishuhudie kwa mbali , ghafla alitokea bondia huyo Thomas mashali akiwa na wenzake wanne akanishika mikono na wenzake kuanza kunisachi nilimputa mikono ili nizuie mifuko ndipo aliponipiga ngumi kali ya kidevuni na kichwani, watu walio karibu walipotugeukia sisi mashali na wenzake waliondoka haraka na kutokomea na simu yangu na kipochi  akiniacha na maumivu ya kidevu.

 

SOMA ZAIDI

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname