20 October 2015

Maguful: ‘Ushindi Wa CCM Ni Wa TSunami’


gombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli.
Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli.
Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM )Dkt John Pombe Magufuli amewaambia wananchi kuwa ushindi wa CCM mwaka huu ni wa Sunami.
Akizungumza na wananchi katika uwanja wa Ihumilo Nkome jimbo la Geita jioni hii Magufuli amesema kwamba Chama cha Mapinduzi kinatarajia kupata ushindi mnono katika uchaguzi mkuu utakaofanyika jumapili ya wiki hii nchini kote.
Amesema kwamba kila anakopita wananchi wanazungumza Magufuli, akitolea mfano Arusha katika majimbo ya Arusha mjini, Monduli na Mbeya sehemu ambayo inadaiwa kuwa ni ngome ya upinzani pamoja na Visiwani Zanzibar sehemu ambayo Chama cha Mapinduzi inakumbana na ushindani mkali kutoka chama cha CUF.
Akizungumzia jimbo la Geita Magufuli amesema kwamba atahakikisha kuwa  jimbo hilo litakuwa jipya ikiwa  wananchi hao watampa ridhaa ya kuchaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano katika uchaguzi mkuu ujao ambao utafanyika jumapili ya wiki hii.Katika mkutano huo Magufuli amewataka wananchi katika kanda hiyo kuachana na imani potofu ya kuwaua albino kwa kudhani kwamba wataweza kupata utajiri  au kuvua samaki wengi suala ambalo amedai halina ukweli wowote.
Katika hatua nyingine Magufulia amemnadi mgombea ubunge ambaye anadaiwa alikuwa ni moja wa marafiki wa mgombea urais wa Ukawa maarufu kama King Msukuma.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname