Akizungumza Ijumaa hii kwenye kipindi cha Uhondo cha EFM, Lulu alisema mama yake alifanya kila njia ili kuhakikisha mtoto wake anakuwa salama.
“Mama yangu ana mapenzi pili ni jasiri,” alisema. “Ni mtu ambaye anaweza kusimama kwa kitu anachotaka kufanya na akafanikiwa. Sio mzazi mwenye mapenzi ya kumharibu mtoto. Hajali wewe ni Lulu wewe ni nani, Lulu mwisho getini, ukiingia ndani wewe ni mtoto,” aliongeza.
“Tumepitia maisha fulani ambayo sio marahisi sana, kwahiyo nyakati tunazo nyingi lakini wakati ambao ulikuwa mgumu sana na akasimama wakati dunia nzima ilikuwa against, ni kitu ambacho kinanifanya niwe proud of her. Kipindi cha kesi yangu ni kipindi ambacho alitukanwa aliongelewa vibaya, ushirikina lakini alikubali akasema vyovyote vile lakini huyu ni mwanangu na akapigana na mpaka leo maisha yanaendelea,” alikumbushia Lulu huku akilia kwa uchungu
No comments:
Post a Comment