WATANZANIA wametakiwa kujifunza kuchangamkia fursa za ajira zinazotolewa na Afrika Mashariki kama ilivyo kwa nchi nyingine.
Kauli
hiyo ilitolewa jana na mgombea wa Urais kupitia Chadema, Edward Lowassa
alipokuwa kwenye kampeni zake zilizofanyika katika uwanja wa Shule ya
Msingi Namanga.
Lowassa
alisema iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, atahakikisha kuwa watanzania wanachangamkia fursa za Afrika
Mashariki kama ilivyo kwa Kenya.
“Napenda
mahusiano ya Afrika Mashariki yawe ya kweli na siyo upande mmoja
unafaidi na mwingine haufaidi,”alisema na kuongeza kuwa:
“Watanzania wakiwa wanapita kwenye mpaka wa Namanga wasisumbuliwe wapite bila shida.”
Sehemu
ya wananchi wa eneo la Kisongo, Jijini Arusha wakiwa wamefunga barabara
kuzuia msafara wa Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, ili waweze
kumsalimia na kumsikiliza, wakati alipokuwa njiani kuelekea eneo la
Ngaramtoni mpaka Namanga, kwenye Mkutano wa Kampeni, leo Oktoba 7, 2015.
No comments:
Post a Comment