Chama
cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ulanga, kimemchagua mtoto wa kwanza wa
aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi), Celina Kombani,
Godluck Mtinga kuwania ubunge katika Jimbo la Ulanga Mashariki.
Katibu
wa CCM wa wilaya hiyo, Mathias Mbogo alisema Mtinga (pichani) aliibuka
kidedea kwa kupata kura 731 kati ya 1,029 zilizopigwa na kupendekezwa
kuwania nafasi hiyo iliyokuwa inawaniwa na mama yake aliyefariki dunia
Septemba 24, mwaka huu nchini India.
No comments:
Post a Comment