Aunt Ezekiel Akanusha Kugombana na Nape
Naomba niwakumbushe jambo
moja kubwa na la msingi ambalo labda mmelisahau. Nchi yetu ni ya
kidemokrasia na inaruhusu kila mtanzania kuwa na imani yake ya kisiasa,
kwani ni haki yake ya msingi.Kiukweli nasikitishwa sana na hii tabia ya
watu kuamini kwamba vijana wanaokiunga mkono chama tawala wamenunuliwa,
wanatukanwa kila siku na kudhalilishwa kana kwamba hawana haki kwenye nchi yao.Mbaya zaidi sasa tunaelekea kwenye kupandikizwa ugomvi na viongozi wetu wa chama, najiuliza ili iweje?
Ndio demokrasia hiyo?
Jioni ya leo kuna clip ya
kutengenezwa, imewekwa, eti mimi nagombana na Katibu Mwenezi wa CCM,
hicho kitu hakijawahi kutokea, sisi hatuna tofauti, najiuliza sasa haya
yote yanatoka wapi?
Kwa nini tusiongee sera tukabaki kwenye kuamua kumpigia tunayemtaka?
Kuna wakati kaka yetu
ambaye ni Mwandishi wa muda mrefu Mdimuz aliwahi kuandika twitter kwamba
kuna demokrasia ya mihemko, nikawa sijamuelewa leo ndio nimemuelewa,
tuongee hoja za msingi, tujibu kwa hoja matusi tusiyape nafasi wala
kuchafuana.
Kuna maisha baada ya
uchaguzi, tusije kushindwa kuangaliana usoni na hii mihemko yetu na
jazba tunazozipa nafasi mpaka tunapandikizana mauongo.
Mungu atubariki sana sisi
watanzania na amani yetu iliyo katika hatari ya kuchafuliwa na
wasiojielewa", Aunt Ezekiel ameandika kwenye ukursa wake wa Instagram
Toka jana clip yenye sauti
inayodaiwa ni kuwa ya Aunt Ezekiel ikimtolea maneno machafu Nape
imekuwa ikisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii hususani Whatsapp
No comments:
Post a Comment