Katika
hali ya kushangaza leo makao makuu ya chama cha democrasia na maendeleo
CHADEMA kimetokea kihoja cha karne baada ya watu wanaodhaniwa kuwa
wanachama wa chama cha mapinduzi kufanya maandamano ambayo
hayakufanikiwa na badala yake kusababisha mwandishi wa gazeti la UHURU
kuingia matatani baada ya kuonekana kuambatana na vijana hao waliokuwa
wanataka kuandamana kutokumtaka Edward lowasa.
Majira
ya saa nne asubuhi vijana kadhaa ambao walikuwa wamevalia sare za chama
cha CHADEMA na mabango kadhaa walionekana wakikatiza makao makuu ya
chama hicho kwa mithili ya maandamano huku wakiwa wanachukuliwa picha na
mwandishi wa gazeti la UHURU pamoja na mpiga picha wa Television ya
STAR TV ambapo baada ya kufika makao makuu ya chama hicho walinzi pamoja
na maafisa wa cham hicho walijipanga na kuwazunguka vijana hao ambao
baadhi walikuwa na boda boda hali iliyowafanya vijana hao kutawanyika
kwa kukimbia na kuvua t shirt za chama hicho ambazo walikuwa wamevalia
juu ya nguo nyingine.
| Baadhi ya kadi ambazo inadaiwa kukutwa nazo mwandhishi huyo |
Katika
purukushani hizo waandishi waliokuwa wanawasindikiza waandamanaji hao
akiwemo mwandishi wa gazeti la uhuru CHRISTOPHER LISSA pamoja na mpiga
picha wa STAR TV waliwekwa chini ya ulinzi wa makamanda wa chama hicho
kuwa kuhusishwa na kupanga tukio hilo ili wapate habari kuwa kuna
maandamano lengo likiwa ni kukichafua chama hicho.
Mara
baada ya kuwekwa chini ya ulinzi akiwemo mmoja kati ya vijana ambao
alionekana kuchoka (TEJA) naye alikamatwa ambapo katika maelezo yake
alikiri kupokea shilingi elfu kumi pamoja na T-SHIRT ya CHADEMA kutoka
kwa vijana hao kwa lengo la kuambatana nao katika maandamano hayo ambayo
hayakuwa halali.
Mwandishi
wa gazeti la uhuru CHRISPHER LISSA wakati akitoa maelezo kwa maafisa wa
chadema alisema kuwa yeye alipokea ujumbe mfupi wa maelezo kuwa
kutakuwa na maandamano kuelekea CHADEMA kupinga alichofanyiwa DK SLAA
ambapo kwa mujibu wa mwandishi huyo aliamua kufikisha ofisini na
kupangiwa kazi hiyo ya kufanya coverage katika maandamano hayo ya leo.
Kwa
mujibu wake anasema kuwa leo aliamua kufikia kinondoni kituo cha
manyanya kutafuta hao waandamaji na ndipo alipokutana na wenzake wa
STAR TV na kisha watu ambao walikuwa wamepanga kuandamana kwalifika
wakiwa na gari na kushuka na kuanza kupeana T-SHIRT za CHADEMA huku
wakiwa ni kama wageni wa eneo hilo wakiulizia makao makuu ya chama kwa
watu wengine.
Anasema
kuwa baada ya kugawiana nguo za chadema huku wakiwa hawasemi wao ni
kina nani na wametumwa na nani walianza kusogea makao makuu ya chama
hicho huku wakiimba na kushiria kuwa kua kitu wanakidai,ambapo ndipo
maafisa wa chama waliamua kuwaweka kati na kufanikiwa kuzima tukio hilo.
Akizngumza
na wanahabari afisa wa chama hicho BONIFACE JACOB amesema kuwa chama
kilipata taarifa siku tatu nyuma kuwa kuna vikao vinakaa chini ya
viongozi wawili wa CCM avikao ambavyo vilifanyika kurasini na ndipo
chama kilijipanga kwa tukio hilo la leo.
Kwa
mujibu wa afisa huyo anasema kuwa mwandishi huyo wa UHURU anahisiwa
kushiriki kupanga maandamano hayo kutokana na kukutwa na kadi zaidi ya
20 feki za chama hicho ambazo walijipanga kujifanya kama zimerudishwa na
wanachama hao kadi ambazo mwandishi huyo amekana kuhusika nazo
No comments:
Post a Comment