Vituko vya uchaguzi 2015!
Mgombea wa nafasi ya udiwani kupitia Chama cha Wananchi (CUF) na
Muunganiko wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Kata ya Mji Mpya
Manispaa ya Morogoro mjini hapa, Kondo Mkutu, ametoa kali ya mwaka baada
ya kuwaita wake zake wawili jukwaani na kuwapatanisha.
Tukio hilo la kushangaza
lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye mkutano wa ufunguzi wa
kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Kaloleni ambapo wahudhuriaji
walihoji kwamba inawezekanaje mgombea wa siasa kuwapatanisha wake zake
katika jukwaa la siasa na wakati sheria za umoja wa nchi zinazounda
Jumuiya ya Madola (nchi zilizotawaliwa na Mwingereza), jambo hilo
halitakiwi kufanyika jukwaani.
Mkutu anayetarajia
kupambana vilivyo na mgombea kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wenslaus
Kalogerezi aliamua kufanya hivyo ili kuwaoneshea wapiga kura kwamba kama
ameweza kuwapatanisha wake zake wawili, Khadija Enzidoli (mke mkubwa)
na Asia Kabwe (mke mdogo) basi hatashindwa kuwapatanisha wananchi wa Mji
Mpya na kuwa kitu kimoja.
“Kama hili limewezekana,
endapo mtanipa kura zenu katika uchaguzi wa mwaka huu, nitawaunganisha
wananchi na kuleta maendeleo,” alisema.
No comments:
Post a Comment