26 September 2015

SIMBA SPORT CLUB YAANZISHA TUNZO YA MCHEZAJI BORA WA MWEZI

Rais wa Simba Sport Klabu Evans Aveva (Kulia) akiwa na afisa Mtendaji Mkuu wa Eaggroup Imani kajula wakati wa Uzinduzi wa tunzo za Mchezaji bora wa Mwezi .
Katika kuongeza morali na kuwazawadia wachezaji wanaofanya vizuri, Klabuya Simba imeanzishaTunzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi kuanzia mwezi wa Septemba 2015. 
Akizungumza jijini Dar es salaam Raiswa Simba Evans Aveva alisema “Uongozi, wanachama na wapenziwa Simba wanathamini mno mchango wa wachezaji katika kuifanya timu  yetu ifanye vizuri, hivyo tumeona ni jambo la busara kuwa klabu  ya kwanza Nchini Tanzania kuwa na tunzo za mchezaji wake bora. Tunaamini kuwaTunzo yaMchezaji bora wa mwezi wa Simba itaongeza ari na kujituma kwa wachezaji wetu. Sisi tukiwa kama viongozi ni kazi yetu ya msingi kuhakikisha  kuwa wachezaji wetu hasa wale wanaojituma  zaidi wanatambuliwa na kuenziwa’’.

Akizungumza jinsi tunzo ya mchezaji bora itakavyoendeshwa, Mkurugenzi Mkuu wa EAG Group ambao ni washauri na watekelezaji wa Masoko na Biashara wa Simba, Imani Kajula alisema “Wanachama na wapenziwa Simba na wapenda michezo ndio watakao kuwa wanachagua mchezaji bora wa mwezi kwa kutuma jina la mchezaji wanayempendekeza kwenda kwenye namba 15460, Ni wale tu ambao wamejiunga na Simba News kupitiamtandaowaVoda na Tigo wataweza kupiga kura kuchagua mchezaji bora wamweziwa Simba’’
Simba News ni huduma iliyoanzishwa na Simba ilikuwapa  wapenzi wa Simba habari mbalimbali za Simba popote pale walipo ikiwemo matokeo, majina ya wachezaji wanaocheza mechi, usajili na habari nyingine za klabu ya Simba. Kujiungana Simba News tuma neno Simba kwenda namba 15460 ni maalum kwa Tigo na Vodacom.

Jinsi ya kumchagua mechezaji bora wa mwezi September 2015.

1. Jiunge na Simba News kwa kutuma neno Simba kwenda namba 15460.

2. Tuma jina la mchezaji kwenda namba 15460.


Kwa maelezo zaidi tembelea www.simbasports.co.tz

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname