Vinara wa biashara Afrika
walipewa tuzo mbalimbali za African Business katika picha ya pamoja.
Kuanzia kushoto ni Daphne Mashile Nkosi, Strive Masiyiwa, Helen Hai na
Mohammed Dewji . hafla ya utoaji wa tuzo hizo ilifanyika hoteli ya Four
Seasons Hotel mjini New York.(Picha na African Business).
Na Mwandishi wetu, New York
MTANZANIA Bilionea Mohamed Dewji amepata tuzo ya Mfanyabiashara Bora wa Afrika wa mwaka 2015, katika kinyang’anyiro cha tuzo za wafanyabiashara bora wa Afrika (African Business Awards 2015).
Dewji maarufu kama Mo alikabidhiwa tuzo hizo usiku wa kuamkia jana mjini New York.
Katika hafla hiyo iliyofanyika katika hoteli
ya Four Season mkabala na jengo la Umoja wa Mataifa (Baraza Kuu) watu
wengine waliopata tuzo ni Aliko Dangote, Daphne Mashile Nkosi, Strive
Masiyiwa na Helen Hai.
MO alimshinda Aliko Dangote ambao walikuwa
kwenye Kategori moja wakiwania tuzo hiyo ya mfanyabiashara bora wa
Afrika, huku wengine walioshindanishwa kwenye kategori hiyo ni CEO wa
Paramount Group, Ivor Ichikowitz, CEO wa Groupe Loukil, Groupe UADH,
Bassem Loukil, na Oscar Onyema DG wa Nigerian Stock Exchange.
Tuzo hizo zimeandaliwa na jarida la African Business .
Pia katika tuzo hizo taasisi kadhaa
zinazofanya vyema bara la Afrika zilitambulika. Taasisi hizo ni pamoja
na kiwanda cha sementi cha Dangote , Guaranty Trust Bank, Abellon Clean
Energy, Nigerian Stock Exchange na taasisi ya bima kwa masoko
yanayochipukia ya BIMA.
Akielezwa wasifu wake katika hafla hiyo, Mo
ameelezwa kama mfanyabiashara aliyefanikiwa kutokana na kuongeza kipato
na ukubwa wa kampuni ya Mohammed Enterprise toka aitwae kutoka kwa baba
yake.
Akiwa mtendaji wa kampuni hiyo, akiwa katika
miaka ya 40 amefanya mabadiliko makubwa katika makampuni mbalimbali ya
umma yaliyoshindwa kujiendesha katika sekta ya kilimo, viwanda na maeneo
ya makazi na viwanda.
Uongozi wake uliwezesha kampuni hiyo ya MeTL
kufanya makubwa kiasi cha kumfanya aingie katika jarida la Forbes la
matajiri wa Afrika.
Majaji waliompa tuzo kwa mwaka huu walisema kwamba uongozi wake
umewezesha biashara katika kampuni hiyo kuchupa kutoka dola za Marekani
milioni 30 hadi bilioni 3.
Akipokea tuzo hizo Dewji alisema kwamba tuzo hiyo ni ishara muhimu kwa
waafrika wote na uwakilishi wa uhakika wa vijana katika masuala ya
ujasirimali.
No comments:
Post a Comment