Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe
Magufuli leo akihutibia moja ya mikutano yake ya kampeni aliyoifanya
katika wilaya za Mbogwe, Bukombe mkoani Geita na Kisha Halmashauri pya
ya Ushetu baadaye mkutano mkubwa wa kampeni uliofanyika mjini Kahama
mkoani Shinyanga ambapo mji huo umetikisika kutokana na umati wa
wananchi waliohudhuria mkutano huo uliorushwa moja kwa moja na kituo cha
Televisheni cha Star TV huku baadhi ya wananchi wakisema CCM ilmeleta
Sunami Kahama.
Akizungumza katika mkutano huo
wakati akiwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi Oktoba 25 mwaka huu ili
kumpigia kura za ndiyo ili awatumikie watanzania katika nafasi ya Urais
na kuongeza kwamba moja ya mambo ambayo serikali yake itashughulikia ni
pamoja na kuhakikisha madereva wanapata mikataba kutoka kwa waajiri wao
ili kuboresha maslahi yao.
Amesema Madereva ni watu muhimu
sana katika sekta ya usafirishaji na wanafanya kazi ngumu sana lakini
maslahi yao hayajaangaliwa kwa makini na kuyaboresha ili na wao ili na
wao waone faida ya kazi yao, Na siyo kuumia bila kipato
kinachowatosheleza katika kuendesha familia zao na maendeleo yao
kiuchumi. hivyo serikali ya awamu ya tano itakayoongozwa na Dk. John
Pombe Magufuli italiangalia pia suala hilo.(PICHA NA JOHN
BUKUKU-FULLSHANGWE-KAHAMA)
No comments:
Post a Comment