
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Dk.
Willibrod Slaa amesema anakwenda Marekani pamoja na familia yake kwa
mapumziko.
Hata hivyo, taarifa zinasema Dk. Slaa amekwishandoka nchini kuelekea Marekani pamoja na familia yake tangu jana jioni.
Huku akiwa Marekani kupumzika na kujiendelea katika kozi fupi katika
tasnia ya Sheria na Lugha, Dk. Slaa amesema nyumba yake itakuwa chini ya
ulinzi wa Jeshi la Polisi.
Akizungumza katika mahojiano yaliyorushwa jana asubuhi na kituo cha
televisheni cha Azam, mwanasiasa huyo amesema akiwa mapumzikoni
Marekani, nyumba yake itakuwa inalindwa na Jeshi la Polisi kutokana na
vitisho ambavyo amekumbana navyo tangu alipoamua kuachia ngazi Chadema
“Ninatishiwa maisha, ni lazima nichukue tahadhari….., ninatishiwa
kupigwa mawe. Ni kweli ninalindwa na usalama,” amesema Slaa akiwa
anahojiwa na mwanahabari nguli, Tido Mhando.
Hata hivyo, Dk. Slaa ambaye ameshawahi kuwa mbunge wa Karatu mkoani
Arusha amesema anashangazwa na taarifa zinazoenea kuwa amelala katika
hoteli ya kifahari ya Serena jijini Dar es Salaam na kuhoji wakati wa
uchaguzi mkuu, 2010, alilala mahali hapo lakini hakuna aliyehoji.
Kuhusu gharama alizotumia kufanya mkutano na wanahabari katika hoteli ya
Serena, Dk. Slaa amesema, alipoenda Marekani katika ziara ya kichama,
alizuru majimbo 13 na hakutumia fedha za Chadema bali marafiki zake
ambao hakuwaweka bayana.
Dk. Slaa amesema licha ya kuwa ng’ambo katika kipindi hiki muhimu kwa
taifa, ataendelea kufuatilia yanayojiri nchini. Ameahidi kurudi kupiga
kura muda ukifika.
Hapo chini Kuna Audio ya Mazungumzo yaliyorushwa jana na Azam Tv wakati akihojiwa na Tido Mhand
No comments:
Post a Comment