Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli
akizungumza huku aliyekuwa mgombea ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi
jimbo la Sikonge Bw. Said Mkumba akionyesha kadi yake ya CHADEMA
aliyokabidhiwa na chama hicho kabla ya kurejea CCM akionyesha kadi yake
hiyo kabla ya kumkabidhi Dr. Magufuli wakati alipotangaza rasmi kurejea
CCM na kukabidhi kadi hiyo kwa Dr. John Pombe Magufuli katika mkutano wa
kampeni uliofanyika leo mjini Sikonge mkoani Tabora.
Dr. Magufuli amewataka viongozi
wa CCM wilaya hiyo na mkoa wa Tabora kushirikiana na Ndugu Said Mkumba
ili kuhakikisha CCM inapata ushindi wa kishindo katika jimbo hilo, Awali
Ndugu Said Mkumba aliuelezea umati wa wananchi waliohudhuria katika
mkutano huo kwamba atazungunguka jimbo zima la Sikonge, Mkoa wa Tabora
na ikiwezekana nchi nzima kuhakikisha anaipigia debe CCM ili ishinde kwa
kishindo katika uchaguzi wa Rais , Wabunge na Madiwani unaotarajiwa
kufanyika mwaka huu Oktoba 25 nchini kote.(PICHA NA JOHN
BUKUKU-FULLSHANGWE SIKONGE)
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli
na Ndugu Said Mkumba wakimnadi mgombea ubunge jimbo la Sikonge Ndugu
George Joseph Kakunda mjini Sikonge leo mara baada ya Said Mkumba
kukabidhi kadi hiyo ya CHADEMA na kurejea rasmi CCM huku akiahidi kupiga
debe la kufa mtu kwa CCM.
No comments:
Post a Comment