10 September 2015

Diamond Platnumz amechaguliwa kuwania tuzo za MTV Europe Music Awards 2015.

diamond 3Bongo Fleva super star Diamond Platnumz ametajwa kuwania tuzo kubwa za kimataifa za MTV Europe Music Awards 2015 [MTVEMA] katika kipengele cha Best African Act.
Wasanii wengine kutoka Afrika wanaowakilisha nchi zao kwenye kipengele hichi ni Aka wa Afrika Kusini, Yemi Alade na Davido kutoka Ghana.
Sababu wasanii wanahitajika watano kukamilisha kipengele MTV imetoa nafasi kwa mashabiki kuwapigia kura wasanii wao ili mmoja awekwe hapo. Majina yaliyootolewa na MTV Ni pamoja na Wiz Kid wa Nigeria, K.O Wa Afrika Kusini, Stonebwoy wa Ghana, Cassper Nyovest wa Afrika Kusini na Dj Arafat wa Cote D’Ivoire.
MTV EMA’s zitafanyika October 25 2015 jijini Milan, Italy. Hii ni mara ya 3 tuzo hizi zinafanyika Italy na mara ya pili kwenye jiji la Milan.
diamond

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname