Mwenyekiti Msaidizi wa
Tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM, Wema
Sepetu akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam juu ya tamasha
na kampeni zao. Kutoka kulia ni Wellu Sengo (Matilda).
Mwenyekiti Msaidizi wa
Tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM, Wema
Sepetu akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam juu ya tamasha
na kampeni zao. Kulia ni Yobnesh Yusuph (Batuli) na kushoto ni Steve
Mengele a.k.a Steve Nyerere wakiwa katika mkutano huo.
Kada wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) na Mratibu wa Tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia
kampeni CCM, Steve Mengele a.k.a Steve Nyerere akizungumza na waandishi
wa habari leo juu ya tamasha hilo.
Mwenyekiti Msaidizi wa
Tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM, Wema
Sepetu (kulia) akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam juu ya
tamasha na kampeni zao. Kutoka kulia ni Wellu Sengo (Matilda) na
Yobnesh Yusuph (Batuli).
Mwenyekiti Msaidizi wa
Tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM, Wema
Sepetu akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam juu ya tamasha
na kampeni zao. Kulia ni Yobnesh Yusuph (Batuli) na kushoto ni Steve
Mengele a.k.a Steve Nyerere wakiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya wasanii na makada
wa CCM ambao watajumuika katika tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015
litakaloipigia kampeni CCM wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya
mkutano na waandishi wa habari.
Baadhi wa aandishi wa habari wakiwasikiliza wasanii hao na waratibu wa tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015.
Na Joachim Mushi, Dar es Salaam
WASANII ambao ni makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameandaa Tamasha kubwa kuzunguka nchi nzima kwa pamoja na kukinadi chama hicho tawala pamoja na Sera zake ili kiweze kushinda Uchaguzi Mkuu onaotarajia kufanyika Oktoba Mwaka huu (2015).
WASANII ambao ni makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameandaa Tamasha kubwa kuzunguka nchi nzima kwa pamoja na kukinadi chama hicho tawala pamoja na Sera zake ili kiweze kushinda Uchaguzi Mkuu onaotarajia kufanyika Oktoba Mwaka huu (2015).
Tamasha hilo
litakalojulikana kama “MAMA ONGEA NA MWANAO 2015″ limeandaliwa na baadhi
ya wasanii makada wa CCM wapatao 250 ambao watazunguka mikoa zaidi ya
10 kukipigia kampeni chama hicho tawala ili kiweze kupewa ridhaa tena na
Wananchi ya kuendelea kuongoza nchi.
Akizungumza leo jijini Dar
es Salaam na waandishi wa habari Mwenyekiti Msaidizi wa tamasha hilo,
Wema Sepetu alisema madhumuni ya tamasha la Mama Ongea na Mwanao 2015 ni
kulinda mazuri yote yalioasisiwa na CCM kupitia viongozi wake akiwemo
Baba wa Taifa Mwalimu Julias Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume.
Msanii Sepetu akiyataja
masuala hayo yalioasisiwa na CCM kupitia viongozi hao kuwa ni pamoja na
amani na utulivu uliopo hadi sasa, maendeleo ya kijamii na kiuchumi
yalioletwa hadi sasa, masuala ambayo yanastahili kuendelezwa na wala si
kubezwa.
Tamasha hilo linajumuisha
wasanii kama Odama, Davina, Wastara Juma, Keisha, Wellu Sengo (Matilda),
Bi. Mwenda, Mama Lolaa, Mama Nyamayao, Herieth Chumila, Thea, Maya,
Chuchu Hans, Steve Nyerere pamoja na wasanii wengine wengi.
Aidha alisema kupitia
tamasha hilo wasanii hao pamoja na wenzao watazunguka katika mikoa zaidi
ya 10 kwa pamoja kufanya kampeni kumnadi mgombea wa urais kupitia CCM,
Dk. John Pombe Magufuli, mgombea Mwenza, Samia Hassan Suluhu pamoja na
viongozi wengine ngazi mbalimbali wanazogombea kupitia chama cha
Mapinduzi.
Madhumuni ya tamasha la
Mama Ongea na Mwanao 2015 ni kulinda mazuri yote yalioasisiwa na CCM
kupitia viongozi wake akiwemo Baba wa Taifa Mwalimu Julias Nyerere na
Sheikh Abeid Aman Karume ambayo bila amani mama awezi kujifungua salama,
Bila mama hakuna familia, amani inapotoweka mama hawezi kukimbia
kilometa kadhaa na kuiacha familia yake, bila mama hakuna ujasiliamali,
mama ni kimbilio la baba, kaka, dada na watoto…ikumbukwe kuwa mama ndio
mpiga kura ndio maana tunasema mama ongea na mwanao,” alisema Wema
Sepetu.
“Na leo hii kuanzia sasa
tunatambulisha kampeni yetu tunayoifanya kuhamasisha vijana, kinamama,
kinababa, mashabiki wetu wale wote wenye sifa za kupiga kura wapige kura
kwa kumchagua kiongozi bora anayetoka Chama Cha Mapinduzi…chagua Dk.
Magufuli, Samia Suluhu, wabunge na madiwani wa Chama Cha Mapinduzi,”
alisema Sepetu.
Aidha wasanii hao
wamempongeza Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Jakaya Kikwete kwa kuongoza vizuri vikao vyote vya chama hicho
hadi kupatikana kwa mgombea bora wa urais kupitia chama hicho (Dk.
Magufuli), hivyo kuwataka wanaCCM wote ambao waligombea na hawakupata
nafasi kuungana na kukitumikia chama.
“…Mimi Wema Abraham Sepetu
nikiwa na baadhi ya wasanii wenzangu ambao tuligombea tunasema muda bado
tunao na siku tunazo kwa kukitumikia chama tukipewa ridhaa kwa njia
yoyote na kwa nafasi yoyote ndio maana hatuja teteleka tupo imara
kuwatumikia wananchi katika nafasi nyingine ndani ya CCM,” alisema
Sepetu.
Imeandaliwa na www.thehabari.com
Imeandaliwa na www.thehabari.com
No comments:
Post a Comment