20 August 2015

SBL YAPELEKA UZINDUZI WA TUZO YA UBORA WA THAMANI KWA WAKAZI WA MWANZA NA MOSHI

Mkazi wa Kona ya Bwiru jijini Mwanza Bw.Godfrey Urio akicheza muziki mara baada ya kuibuka mshindi wa shindano la “Serengeti Masta” wakati wa kusherekea uzinduzi kampeni ya tuzo ya dhahabu ya ubora wa thamani ya Monde Selection ambapo kwa mwaka huu bia ya Serengeti Premium Lager toka SBL imejinyakulia medali tatu za dhahabu kutokana na ubora wake. Hafla hiyo ambayo ilikua mahususi kwa wakazi wa kanda ya ziwa, ilifanyika katika baa ya “The dreams” iliyopo Kona ya Bwiru jijini Mwanza. Shindano la “Serengeti Masta” litafanyika Tanzania nzima na kuibua Mshindi mmoja kwa kila kanda na mwisho kumuibua wa kitaifa. Kauli mbiu ya kampeni hii ikiwa ni “TUNAIJUA BIA NA SERENGETI PREMIUM LAGER NDIO YENYEWE”.

Wafanyakazi wa kampuni ya Serengeti Brewieries Limited wakiwa na Mabalozi wa kinywaji hicho wakati wa  kutambulisha Tuzo ya Dhahabu ya Monde inayotambulika kimataifa baada ya bia ya Serengeti Premium Lager kukidhi viwango vya juu vya ubora katika hafla iliyofanyika katika Baa ya Oriental ,Majengo mjini Moshi mwishoni mwa wiki.

Meneja mipango ya biashara, matukio na uhamasishaji  wote wa kampuni ya Serengeti Breweries Limited Bw. Denis Tairo akizungumza na wateja wa bia ya Serengeti Premium Lager wakati wa uzinduzi kampeni ya tuzo ya dhahabu ya ubora wa thamani ya Monde Selection kwa wakazi wa kanda ya ziwa jijini Mwanza ambapo bia ya Serengeti Premium Lager ya SBL imetuzwa medali tatu za dhahabu kutoka kwenye viwanda vyake vyote vitatu; cha Dar es salaam, Mwanza na Moshi kwa mwaka 2015. Uzinduzi huo ulifanyika katika baa ya “The dreams” iliyopo Kona ya Bwiru jijini Mwanza.


Meneja mipango ya biashara, matukio na uhamasishaji  wote wa kampuni ya Serengeti Breweries Limited Bw. Denis Tairo akikabidhi zawadi ya polo shirt na kofia kwa mkazi wa Kona ya Bwiru jijini Mwanza,Godfrey Urio mara baada ya mkazi huyo kuibuka mshindi wa shindano la “Serengeti Masta” wa baa ya “The dreams” ya jijini Mwanza wakati wa kusherekea uzinduzi kampeni ya tuzo ya dhahabu ya ubora wa thamani ya Monde Selection ambapo bia ya Serengeti Premium Lager imetuzwa medali tatu za dhahabu kwa mwaka huu wa 2015. Shindano hilo litafanyika Tanzania nzima na kuibua Mshindi mmoja kwa kila kanda na mwisho kumuibua wa kitaifa. Kauli mbiu ya kampeni hii ikiwa ni “TUNAIJUA BIA NA SERENGETI PREMIUM LAGER NDIO YENYEWE”.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname