Mawakili wa kampuni ya Web Advocates & Solicitors wa nchini
Uganda wamemwandikia barua mzazi mwenza wa Icon wa Bongo Fleva Africa,
Diamond Platinumz, Zari Hassan ‘Zari The Boss Lady’wakihitaji mwanaye
Latifa ‘Tiffah’ afanyiwe vipimo vya DNA ili kuthibitisha mzazi wa mtoto
huyo ikiwa ni sehemu ya madai ya mpambe wa tajiri Ivan aitwae King
Lawrence.
King amedai kuwa yeye ni baba wa mtoto huyo. Mapema mwezi huu
Zari alijifungua mtoto wa kike, Tiffah ambaye inadaiwa kuwa ni wa
Diamond, lakini Lawrence ameibua hali ya wasiwasi kwa kudai yeye ndiye
baba wa mtoto huyo na asingependa kuona analelewa na mwanaume mwingine.
Barua hiyo ya Agosti 14 iliyoandikwa na mawakili hao kwa Zari,
imemtaka kutoa ushirikiano ndani ya siku saba za kazi ili kufanyika kwa
vipimo hivyo vitatu tofauti ya DNA nchini Uganda, Afrika Kusini na
Marekani ambavyo vitagharimiwa na mdai huyo. Mawakili hao wametishia
kuchukua hatua zaidi kama Zari atagomea ushirikano.Jambo la kutia shaka na kuona kwamba pengine Lawrenc anatafuta ‘Kick’ kupitia Diamond, ni kwamba hivi juzi tu jamaa huyo alidai mtoto huyo baba yake ni rafiki yake Ivan, leo hii anaibuka na kudai mtoto ni wake.
No comments:
Post a Comment