Tumekuwa
na mazoea kuona video za wasanii wakubwa Tanzania kufanyika nje ya
Tanzania, AY amepanga kuja na kitu tofauti baada ya kufanya video ya
Zigo hapahapa Tanzania na kuwa kinyume na watu waliofikiria kuwa
atafanya nyimbo hii nje ya nchi.
Akizungumza katika 255 ya XXL Ay atoa sababu za kuifanya video hii Tanzania chini ya Mtayarishaji Nisher. Ay amesema "Nilikuwa
nataka nimpatie jukumu mtanzania mwenzangu, pili nataka tutumie
location za Tanzania na ya tatu ni kwamba sipendi kufanya kitu ambacho
kila mtu atategemea ntafanya kitu cha aina flani, let say mi nikisema
nafanya video kwa mtu ambae anafikiria haraka haraka atasema naenda
kufanya South Afrika kwa Godfather" alimaliza AY
No comments:
Post a Comment