Staa wa filamu za bongo, Wema Sepetu ‘Madam’.
HAKUNA
mwanzo usiyokuwa na mwisho! Huu ni usemi pekee ambao umejidhihirisha
kwa Mkurugenzi wa Endless Fame Production na mbunge mtarajiwa wa Viti
Maalum mkoani Singida kwa leseni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wema
Isaac Sepetu baada ya kumwangukia aliyekuwa shostito wake, Kajala
Masanja ‘Kay’.
Wema na Kajala wamekuwa na bifu zito lililokuwa
likichukua sura mpya kila kukicha kufuatia wawili hao kutokusameheana,
kutukanana na kukashifiana ambapo Wema alifikia hatua ya kumwita
mwenzake ‘bogasi’ na yeye (Kajala) akamwita chizi.
Tukio la Wema
kujishusha na kutoa kauli ya kusema yuko tayari kumsamehe Kajala aliitoa
mbele ya mwandishi wetu, Julai 15, mwaka huu ndani ya Ofisi za gazeti
hili, Bamaga-Mwenge jijini Dar.
Kajala Masanja ‘Kay’.
No comments:
Post a Comment