Kituo cha Polisi Bunju B kikiteketea baada ya kuchomwa na wananchi wenye hasira kali.
Moshi mkubwa kutoka eneo hilo la kituo.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Bunju A wakiwa barabarani.
Barabara zikiwa zimefungwa.
Baadhi ya wakazi wa Bunju leo wamevamia na kukichoma moto Kituo cha
Polisi Bunju A baada ya polisi kufyatua mabomu ya machozi na risasi za
moto kuwatawanya wananchi waliofunga barabara baada ya mwanafunzi wa
darasa la nne Shule ya Msingi ya Bunju A kugongwa gari na kufariki leo
asubuhi.Polisi walilazimika kukimbia na gari lao baada ya kuona wananchi wanawazidi nguvu kwa kurusha mawe na kukiacha kituo hicho bila ya ulinzi ndipo wananchi walipokivamia kituo kuvunja milango na kuwatoa wahalifu waliokuwa wakishikiliwa na kisha kukichoma moto.
Wananchi hao walilazimika kufunga barabara ili kushinikiza kuwekwa matuta katika eneo hilo la barabara.
Polisi wamesema kuwa wameongeza nguvu katika eneo la Bunju A kukabiliana na wananchi wa eneo hilo kufuatia tukio hilo.
Credit: EATV
No comments:
Post a Comment