Stori kubwa leo hii ni aliyekuwa winga wa Simba SC, Ramadhan Singano
‘Messi’ kusaini mkataba wa miaka miwili katika klabu ya Azam fc, ikiwa
ni siku mbili tu tangu TFF wavunje mkataba wake na Wekundu wa Msimbazi.
Messi amesaini mkataba mnono kwa dau la milioni 50 na atakuwa analipwa mshahara wa Milioni 2 kwa mwezi.
Kabla ya kuingia katika mgogoro wa kimkataba na Simba, Wekundu wa
Msimbazi walitaka winga huyo asaini mkataba wa miaka miwili kwa dau la
milioni 30 na mshahara wa milioni 1.5, lakini alikataa.
No comments:
Post a Comment