Rais wa Marekani, Barach Obama (kushoto), mkewe Michelle Obama (kulia) na katikati ni Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.
Sifael Paul na mtandao
Ni Obama kila kona! Muda wowote kuanzia
leo wananchi wa Kenya watashuhudia kutua kwa Rais wa Marekani, Barack
Hussein Obama, nchini humo huku stori kubwa ikiwa ni ulinzi uliowekwa
kwa hofu ya kundi ‘haramu’ la ugaidi la Alshabaab, Ijumaa linakupeleka hadi kwa majirani zetu hao.
Ziara ya Obama ambaye ana asili ya Kenya
kutokana na baba yake, Hussein Obama kuwa ni raia wa Kenya, itakuwa na
ulinzi ambao hata mwenyeji wake, Rais Uhuru Kenyatta hana.
VIKOSI VYA ULINZI
Habari kutoka nchini humo zilidadavua
kwamba, vikosi vya ulinzi vya Marekani, CIA, FBI na kile cha siri cha
Secret Service vilitua nchini humo miezi kadhaa na kuungana na majeshi
ya Kenya ili kuweka mambo safi.
Meli iliyobeba ndege za kivita.
MANOWARI ZA KIVITA
Ilielezwa kwamba, meli na manowari za
kivita vimepiga kambi eneo lote la pwani ya nchi hiyo katika Bahari ya
Hindi, lengo likiwa ni kuimarisha usalama wa kiongozi huyo mkubwa
duniani pamoja na jopo la wafanyabiashara atakaoandamana nao.
B52 YAEGESHWA PWANI
Ilielezwa kwamba, jeshi la kwenye maji
la Marekani limejikita Bahari ya Hindi kwenye ukanda wote wa Afrika
Mashariki kujiandaa kuzuia shambulizi la kivita wakiwa na silaha nzito
ndani ya ndege ya B52 ambayo imeegeshwa pwani ya nchi hiyo.
KAMERA, SATELAITI ZAFUNGWA
Ilisemekana kwamba, Jeshi la Kenya
wameweka doria kwenye Jiji la Nairobi ambalo limetulia tuli huku
likimulikwa kwa kamera maalum na satelaiti za kijeshi, barabara
kufanyiwa usafi na nyingine kufungwa huku bendera za Kenya na Marekani
zikiwa zimepamba Jiji la Nairobi.
AIR FORCE ONE
Imedadavuliwa kwamba, Obama atatua na
ndege ya Rais wa Marekani ya Air Force One aina ya Boeing 747-200B kisha
atapokelewa na gari analotumia Marekani ambalo lilitangulia kuwasili
Kenya.
UWANJA WA NDEGE
Ilielezwa kwamba, kwenye Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta atakaotua Obama, kumejaa ndege za Jeshi
la Marekani na hauruhusiwi kutumiwa na ndege nyingine za biashara.
Hali ndivyo ilivyo kwa viwanja vingine
pamoja na bandari, hakuna biashara inayoendelea hadi kiongozi huyo
amalize ziara yake nchini humo.
Gari na helikopta zisizopenya risasi.
MAMLAKA YA ANGA
Ilielezwa kwamba, Mamlaka ya Anga ya
Marekani na Makao Makuu ya Jeshi hilo Pentagon wanafanya kazi kama siafu
kuhakikisha anga lote lipo shwari.
Kuna taarifa kwamba, wafanyakazi wote
serikalini wasiohusika na usalama na ziara hiyo watakuwa miguu
atakapowasili Obama kwani hawataenda kazini.
Kuhusiana na ulinzi wa Kenya, hata nchi
za Tanzania, Somalia, Eritrea, Uganda, Rwanda na Burundi nazo
zinamulikwa kusije kukatokea lolote.
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.
KILICHOMLETA
Akiwa nchini Kenya, Obama atafanya
mkutano na Rais wa Kenya, Uhuru na baada ya hapo wawili hao watahudhuria
Kongamano la Ubunifu wa Kibiashara Ulimwenguni la 2015 linalofanyika
kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Nairobi.
Hii itakuwa ziara ya tatu ya Obama Afrika baada ya mwanzo kutembelea Ghana, baadaye Senegal, Afrika Kusini na Tanzania.
MAUAJI YA AL-SHABAAB
Ulinzi huo umekuja kufuatia matukio ya
mauaji ambayo yamekuwa yakifanywa na Al-shabaab ambao walihusika na
mauaji ya wanafunzi 148 katika Chuo Kikuu cha Garissa na shambulizi la
mwaka 2013 la Jengo la Biashara la Westgate ambapo takriban watu 67
waliuawa.
Al-shabaab wamekuwa wakifanya
mashambulizi ya mara kwa mara kwenye maeneo mbalimbali ya Kenya yaliyo
karibu na mpaka wa Somalia, wakidai lazima vikosi vya Kenya viondoke
nchini Somalia ndiyo maana Marekani wameamua kuweka ulinzi mkali kuliko
ule wa Tanzania alipotua Obama mwaka 2013.
KIJIJINI KOGELO
Wakati hayo yakiendelea, inaelezwa
kwamba, wakazi wa kijiji anakotoka mzazi wa Rais Obama, Kogelo,
Magharibi mwa nchi hiyo, wanaamini kuwa kiongozi huyo atawatembelea
kijijini hapo hivyo kwao ni hatua kubwa kwani atazidi kuwaboreshea
maisha.
Kogelo ni kijiji kidogo alikozaliwa mzee
Hussein Obama. Kijiji hicho hakikuwa kikijulikana wala kuwa na huduma
muhimu kama maji na umeme, kama vijiji vingine nchini humo, hadi pale
Barack Obama alipochaguliwa kuwa seneta ambao mwaka 2006 alifika
kijijini hapo na kusaidia mambo mengi. Hivi sasa kijiji hicho kina
umeme, barabara ya lami na shule.
Obama na Bibi yake.
KWA MARA YA KWANZA
Obama amepanga pia kutembelea Makao
Makuu ya Umoja wa Afrika yaliyo Addis Ababa, Ethiopia ikiwa ni ziara ya
kwanza kwa Rais wa Marekani kuzuru umoja huo tangu kuasisiwa kwake
No comments:
Post a Comment