Sitti Mtemvu.
HAPATOSHI! Vita kali ya
kugombea ubunge imezuka katika familia ya Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu
kufuatia watoto wake wawili, Lulu na Sitti Abbasi Mtemvu ambao kwa
pamoja wamechukua fomu ya kugombea ubunge viti maalum kupitia kundi la
umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa Morogoro.
Lulu Mtemvu.
Watoto hao wazaliwa wa
mkoani Morogoro waliochangia baba, kwa nyakati tofauti wiki iliyopita
walitinga ofisi za UVCCM Mkoa na kuchukua fomu hizo kimyakimya.
Mashuhuda wa tukio hilo
walipenyeza ubuyu kuwa Lulu ndiye alikuwa wa kwanza kuchukua fomu hiyo
na siku iliyofuata Sitti aliyeongozana na mama yake mzazi Mariam Mtemvu
walitinga kwenye ofisi hizo na kuchukua fomu hiyo huku mama yake akibeba
jukumu la kupiga picha za tukio hilo.
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM
Mkoa wa Morogoro, lgnas Said Kinywa alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo
na kudai kuwa kigezo kikuu cha nafasi hiyo ni kwa mwanachama kuwa na
kadi na kutozidi umri wa miaka 30.
Lulu anayeishi maeneo ya
Kiwanja cha Ndege alithibitisha kuchukua fomu na mdogo wake, akidai ni
demokrasia mpya katika familia yao, lakini Sitti aliyeachia ngazi ya
umalkia wa urembo nchini (mwaka 2014) kwa kashfa ya kudanganya umri
hakupatikana kupitia simu yake ya mkononi iliyokuwa ikiita bila
kupokelewa.
No comments:
Post a Comment