21 July 2015

NAPE AMRUSHIA KOMBORA LOWASSA , ASEMA CCM IMEWEZA KUYAZUIA MAFURIKO KWA MIKONO


Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimejigamba kwamba kimeweza kuzuia ‘mafuriko’ kwa mikono huku kikiwatakia kila la kheri baadhi ya makada wake waliotangaza kutogombea kupitia chama hicho pamoja na wale waliokihama na wanaotaka kukihama.Mwishoni mwa wiki iliyopita waliokuwa madiwani jimbo la Monduli kupitia CCM mkoani Arusha, walitangaza kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), huku wabunge wa viti maalum, Ester Bulaya na James Lembeli aliyekuwa Mbunge wa Kahama wakitangaza kutogombea kupitia chama hicho
Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akizungumza na mtandao huu jana alisema CCM hakina uwezo wa kuzuia mtu anayetaka kukihama kwa sababu hiyo ndiyo demokrasia.  


BOFYA KUSOMA YOTE

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname