DU!
Kazi kwelikweli! Habari ya mjini kwa sasa ni mtoto mzuri Bongo Movies,
Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ kuwania Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida
kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), lakini nyuma yake kuna habari
zinazodai kuwa mrembo huyo ameingiwa na hofu ya kukatwa jina kama
ilivyotokea kwa Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa aliyekuwa mmoja
wa watia nia ya kugombea urais, Amani lina mkanda kamili.
Lowassa
alikuwa miongoni mwa makada 33 kati ya 38 walioenguliwa na Kamati ya
Maadili ambayo ilipitisha majina matano pekee katika kikao cha Kamati
Kuu, Halmashauri Kuu na baadaye Mkutano Mkuu kupitisha Mbunge wa Chato,
Dk. John Pombe Magufuli kuwa mgombea urais kwa Tiketi ya CCM.
No comments:
Post a Comment