Staa wa Bongo fleva, Emmanuel Elibariki, ‘Nay wa Mitego’.
NI shidaah! Siku chache baada ya Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Ngoyai
Lowassa (pichani) kukaribishwa katika Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa) kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao, mastaa mbalimbali Bongo wameamua na
wengine kushawishiwa kumfuata wakiamini katika uwezo wake kiuongozi,
Amani limenasa mpango mkakati kamili.
Chanzo makini kililieleza gazeti hili kwamba mastaa wote waliokuwa
wakimuunga mkono Lowassa wakati akiwania kuteuliwa na Chama Cha
Mapinduzi (CCM) kupeperusha bendera ya chama hicho katika nafasi ya
urais na baadaye jina lake kukatwa kabla ya kufikishwa Kamati Kuu (CC),
wameamua kuhamia Ukawa kumfuata mwanasiasa huyo aliyejiunga huko kupitia
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
TUJIUNGE NA CHANZO
“Moto huku Ukawa umewaka. Yale makundi mawili ya M4C (Movement For
Change- Chadema) na 4 U Movement (Kundi la Marafiki wa Lowassa) sasa
yameingia kazini. Mkakati maalum umeandaliwa kuhakikisha kila mwenye
ushawishi katika jamii anafikiwa, wakiwemo wasanii wa sanaa mbalimbali.
“Wameanza na wasanii waliokuwa nyuma ya Lowassa kwa sababu wanaamini
wana wafuasi wao, ambao watashawishiwa wawashawishi hao watu wao
wawaunge mkono katika kuhakikisha wanaing’oa CCM madarakani,” kilisema
chanzo hicho.
Wema Sepetu.
WEMA AKARIBISHWA
Chanzo hicho kimeweka wazi kuwa licha ya wasanii kwa jumla, lakini pia
mastaa wenye mvuto mkubwa kwa jamii watafuatwa wao rasmi, kama
ilivyotokea majuzi ambapo mwigizaji Wema Isaac Sepetu alifuatwa na 4 U
Movement (Team Lowassa) kushawishiwa kujiunga na Team Lowassa.
Wiki iliyopita Wema alitoswa katika kura za maoni za kuwania Ubunge wa
Viti Maalum (UWT-CCM) Mkoa wa Singida kwa kushika nafasi ya nne, lakini
akapokewa kwa kishindo katika mapokezi yaliyojaza watu jijini Dar.
“Yaani Wema hivi karibuni aliitwa na watu wa Lowassa kwenye hoteli moja
maarufu jijini Dar ambapo ajenda kubwa ni yeye kuungana na Ukawa kwa
vile wanaamini ana mashabiki wengi,” kilisema chanzo hicho.
HUYU HAPA WEMA
“Ni kweli, juzi nilipigiwa simu na watu waliojitambulisha kuwa ni Team
Lowassa, wakasema wana mazungumzo na mimi, ilikuwa tukutane Jumanne,
lakini nilikuwa na shughuli nyingine nikashindwa kwenda.
“Tulikubaliana tukutane jana, lakini sijaelewa hasa ajenda ni nini na
kwa maana hiyo siwezi kusema lolote kwa sasa kama ninaenda Ukawa au la,”
alisema muigizaji huyo, alipozungumza na gazeti hili.
Jacquiline Wolper.
WOLPER ACHOCHEA
Kana kwamba haitoshi, staa mwingine wa filamu za Kibongo, Jacqueline
Walper Massawe ambaye tangu awali alijitoa muhanga kufa pamoja kisiasa
na mbunge huyo wa Monduli, anatajwa kuwa kinara wa kampeni katika
mitandao mbalimbali ya kijamii akiweka wazi kuwa atamfuata Lowassa
popote atakapokwenda kwani ni shabiki wake mkubwa.
Aunt Lulu.
AUNTY LULU RASMI UKAWA
Ahadi kama hiyo ilitolewa pia na mwanadada Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’
aliyetangaza kujiunga rasmi na Ukawa kwa sababu ya Lowassa.
Kala Jeremiah.
Mastaa wengine ambao wamemfuata Lowassa Ukawa ni pamoja na Deogratius
Shija, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Kala Jeremiah, Khalid
Ramadhan ‘Tunda Man’, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’, Elizabeth Michael
‘Lulu’ na Bahati Bukuku
No comments:
Post a Comment