Diamond Platnumz Akiojiwa na Clouds FM kuhusu Video aliyopost jana ikionyesha Jokate Akicheza Wimbo wake na Kuandika "Mbona Bado, Mtanyooka tu".Amesema
kuwa yeye amempost kwa nia nzuri tu na si kumzalilisha amedai yeye mara
nyingi huwa anawapost watu wakicheza nyimbo zake hivyo kumpost Jokate
kwake ni Kawaida...
Pia ameulizwa kuhusu maneno aliyotumia kwenye video hiyo kuwa ni ya
kichokozi Diamond akadai kuwa yeye ni Mswahili wa Tandele kuandika
Maneno haya ni kawaida kwake kwani amekuwa akiyatumia katika post zake
mbali mbali....lakini leo ametumia kwa Jokate basi watu wengine
wamepanic.....
Mwisho Diamond Akafunguka ya Moyoni kuhusu Jokate na Kusema kuwa si
mzalendo kwa vile anajidai kumpongeza leo baada ya kushinda wakati kabla
ya kushinda yeye na wenzake walikuwa Bize wakishawishi watu wampigie
kura Davido...Amedai hata siku moja hakuwahi kumposti kwa page zake
kumpa sapoti hivyo asijadai leo kulia lia....
‘’Nikasikia kuwa kasema kuwa ndiyo maana wanaogopa kusapoti wasanii wa
Tanzania kwa sababu wakisapoti wanadhalilishwa yeye mpaka naenda
kuchukua tuzo ya Mtumbuizaji Bora yeye amenisapoti nini hajawahi
kunipost hata tuzo moja sasa hivi ndiyo anajishaua eti ananipa hongera
kwa tuzo ningemuona wa maana angepost watu wapige kura na kuwahamasisha
ili ushindi urudi nyumbani lakini kwa chuki alizojazwa pasipo na sababu
na roho mbaya aliyowekwa na watu imemfanya ashindwe kunipost na
kutengeneza chiki za chinichini wakidhani wakiwapigia kura Wanageria
mimi nitakosa tuzo Mungu amewalaani mimi nimeshinda halafu anajifanya
anatoa hongera eti wanasapoti muziki wa Tanzania au kwasababu wameona
tuzo imekuja ndiyo wanajifanya wanatoa hongera tuache unafiki,’’alimalizia Diamond
No comments:
Post a Comment