Jeshi
la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema limefanikiwa
kuwakamata majambazi watano wanaodaiwa kuhusika na tukio la uvamizi
katika kituo cha polisi cha Stakishari kilichopo Ukonga. Kamanda wa
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema majambazi
hayo yamekamatwa Mbagala ambapo katika tukio hilo pia wamekamata pia
fedha shilingi milioni 170 na bunduki 16 miongoni mwao ni zile
zilizoibiwa katika kituo cha Stakishari.
No comments:
Post a Comment