10 July 2015

FAMILIA ZA WAGOMBEA URAIS CCM VILIO.

Mwenyekiti wa CCM, rais Jakaya KikweteSi mchezo! Baada ya Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia na kuridhia majina matano ya wanachama wake walioomba kuteuliwa kuwania Urais katika uchaguzi wa Oktoba mwaka huu, baadhi ya familia za wagombea hao zilizo mjini hapa zimejikuta zikiangua vilio huku zile za waliopenya Tano Bora ziliripuka kwa furaha. Habari zilizolifikia gazeti hili zinasema kuwa familia mbili za wagombea tofauti zilizofikia katika hoteli moja yenye hadhi iliyo mjini hapa, zilijikuta zikiungana kwa furaha baada ya kubaini watu wao wamepenya katika hatua hiyo ngumu ya uteuzi. 

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname